Thursday, October 11, 2007

Dimbani na Toto Africa leo

Yanga leo inajitupa tena dimbani kuchuana na Toto Africa ya Mwanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom itakayopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri huko Morogoro.

Huu utakuwa ni mtihani wa pili kwa kocha Jack Chamangwana ambaye alianza vizuri kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa wiki iliyopita.

Toto Africa na Yanga zinalingana kwa pointi (6 kila moja).

Ushindi kwa Yanga leo kwa namna fulani utatuliza 'machafuko' yaliyotanda Jangwani kufuatia kujiondoa kwa mfadhili wa klabu hiyo Yusuf Manji.

Ukitaka kujua kinachoendelea uwanjani ndani ya dk.90 tafadhali ungana nasi hapo chini katika comments.

Kila la heri Yanga.


10 comments:

Anonymous said...

Tulio mbali, bado tunafuatilia kwenye comments..!

Anonymous said...

Tunaongoza kwa bao 1 hadi sasa

Anonymous said...

Tunaongoza kwa bao 1 hadi sasa ni dk 50

Anonymous said...

Wow, saafi....

Anonymous said...

Dk 58 tumepata bao la pili limefungwa na Fred Mbuna

Anonymous said...

Kipa wetu Ben Haule ameokoa penalti dk 80. Bado ni 2-0

Anonymous said...

Mpira umekwisha, tumeshinda 2-0.

Kipa Haule alipewa red card dk88, hivyo beki Fred Mbuna alikaa golini ktk dk mbili za mwisho.

Kwa ushindi huo sasa tuna pt 9.

Anonymous said...

asante sana anoni hapo juu kwa kutupa habari za klabu yetu kwa haraka sana. Nadhani Chamangwana anadawa ya Yanga kushinda tumtumie vizuri kuliko kukimbilia wa njee

Anonymous said...

Duh, safi sana. Tunashukuru CM kwa kutupa habari za timu yetu, 'live' toka uwanjani. Otherwise ingebidi tusubiri magazeti ya mtandao kesho.

CM said...

Nawashukuru wadau wote ambao mlikuwa pamoja nami muda wote wakati nawatumia kilichokuwa kinaendelea uwanjani.

Ushirikiano wenu ni muhimu katika kuendeleza blog yetu hii.

Nawatakia kila la heri katika shughuli zenu.