Wednesday, October 17, 2007

Kibaruani na Moro United leo

Ligi Kuu ya Vodacom leo itaendelea tena ambapo Yanga itajitupa uwanjani kupambana na Moro United kwenye Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro.

Moro United inayoundwa na vijana wengi, inatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Yanga ambayo leo itawakosa wachezaji wake kadhaa wakiwemo Ben Mwalala, Athumani Iddi na Kabanda kwa sababu mbalimbali.

Yote juu ya yote tunaitakia heri Yanga katika mchezo wa leo.

Kama kawaida kama mambo yatakwenda vizuri, cheki hapa chini katika comments ili upate kinachoendelea ndani ya dakika 90 kwenye uwanja wa Jamhuri.


4 comments:

Anonymous said...

Kwa jinsi Simba wanavyojua fitna, nahisi leo wataanza kuwatafutia kadi wachezaji wetu ili wasicheze next wednesday. Wanawaogopa sana Mrisho Ngasa na Abdi Kassim. Tusipoangalia watafanya namna. Najua pia walikuwa wanapiga hesabu Kabanda asiwepo, nadhani wamefanikiwa.

Anonymous said...

Hadi mapumziko 0-0.
Mnisamehe leo connection sio nzuri. Samahani kwa ku-delay

Anonymous said...

Mpira umemalizika kwa sare ya 0-0

Anonymous said...

Daah, shukrani kwa matokeo lakini ...