Wednesday, October 17, 2007

Mgogoro Yanga sasa basi!

Ule mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya klabu ya Yanga unaelekea kumalizika baada ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega kuomba radhi wale wote aliowakosea kutokana na matamshi yake aliyotoa wiki iliyopita.

Kwa upande mwingine, mfadhili wa klabu hiyo Yusuf Manji naye ameiandikia barua Yanga akitangaza kuendelea kuifadhili klabu hiyo na kuomba mkataba mpya uandaliwe haraka ili aweze kuweka sahihi.

Aidha Madega pia alitangaza kuondolewa kwa zuio la mahakama kwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo Lucas Kisasa kufuatia jitihada zilizofanywa na uongozi huo.

Hii ni habari njema kwa wana Yanga hasa tukiwa tumebakiza wiki moja tu kabla hatujapambana na Simba kwenye ligi.


No comments: