Wednesday, October 17, 2007

Mwalala kuikosa Simba?

Mshambuliaji wa Yanga Ben Mwalala huenda akalikosa pambano la watani wa jadi endapo kadi nyekundu alioyopewa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar itaripotiwa kuwa ni kutokana na kumtukana mwamuzi.

Mwamuzi wa mchezo huo Peter Mjaya alimwonyesha kadi nyekundu Mwalala kutokana na mchezaji huyo kumtolea lugha chafu mwamuzi huyo. Awali katika mchezo huo, Mwalala alikuwa tayari amepewa kadi ya njano kutokana na kufanya madhambi.

Wadadisi wa mambo ya soka wanasema endapo atapatikana na hatia basi Mwalala anaweza kufungiwa mechi 3 hadi 6.


Tusubiri tuone kamati ya mashindano ya TFF itaamua nini.


1 comment:

Anonymous said...

Maoni yangu kuhusu kitendo ch Mwalala yanafanana na yele niliyoyatoa kuhusiana na kufungiwa kwa Athumani Iddi Chuji. Ni upuuzi kwa mchezaji kumtolea lugha chafu mwamuzi huku ukijua kuwa kwa kufanya hivyo, si tu hutabadili uamuzi aliokwisha kuutoa, bali pia utaiathiri timu endapo utapewa kadi. Ni vizuri uongozi ukaanza kuwabana wachezaji wanaopewa kadi za kijinga kwa kuwakata mishahara. Timu nyingi za Ulaya zinafanya hivi. Fikiria ni jinsi gani timu iliathirika baada ya Mwalala kutolewa.