Tuesday, October 23, 2007

Lazima mnyama alale kesho!!

Bila shaka wengi wetu tunasubiri kwa hamu pambano kubwa la msimu huu dhidi ya Simba hapo kesho. Lakini kitu ambacho wengi wetu inabid tujiulize ni kwanini kwa miaka zaidi ya 4 hatujashangilia ushindi dhidi ya Simba? (Mara ya mwisho ilikuwa Aprili 20, 2003 ambapo Simba ililala kwa 3-0)

Ni kweli inasikitisha kuona tunakuwa wanyonge kila mwaka na hata siku timu yetu ikicheza vizuri huwa tuaambulia sare tu.

Kwa sasa Yanga inaingia kwenye pambano hili ikiwa imeandamwa na mikosi ya wachezaji wake 3 kufungiwa na TFF - Ben Mwalala, Benjamin Haule na Athumani Iddi. Pia Yanga ina orodha ya wachezaji majeruhi - Said Maulid, James Chilapondwa. Aidha kikosini hicho kitawakosa Abdi Kassim na Nadir Haroub 'Cannavaro' ambao wameomba ruhusa. Inasemekana Edwin Mukenya amesimamishwa kwa muda na uongozi wa klabu hiyo.

Lakini pamoja na kukosekana kwa wachezaji hao, bado tuna kikosi imara cha ushindi hiyo kesho hasa kwa vile tunayo sababu na nia ya kumfunga Simba. Miaka yote washinde wao tu? Kwani wametuzidi nini?

Kama alivyoandika mwandishi mmoja kwenye gazeti la Yanga Imara kwamba mashabiki wa Yanga wamechoka kulala mapema kila siku wanapokutana na Simba ndani ya miaka hiyo 4 na ushee. Katika kipindi chote hicho hadi mpambano wa kesho, Yanga tayari imepokea vipigo mara 8 na hata ikicheza vizuri inaambulia sare tu.

Tukiwa tunaelekea kwenye mpambano mkubwa dhidi ya Simba hapo kesho, hebu tuangalie msimamo wa ligi hadi hivi sasa;P W D L F A PTS
1 PRISONS 9 7 2 0 18 6 23
2 POLISI MORO 9 4 4 1 9 3 17
3 KAGERA SUGAR 9 3 4 2 8 5 13
4 JKT RUVU 9 3 4 2 8 6 13
5 YANGA 9 3 3 3 6 4 12
6 MTIBWA SUGAR 9 3 3 3 6 8 12
7 SIMBA 9 2 5 2 7 6 11
8 MORO UNITED 9 2 5 2 3 3 11
9 TOTO AFRICA 9 2 4 3 6 8 10
10 ASHANTI UNITED 9 2 4 3 3 6 10
11 COASTAL UNION 9 2 3 4 4 7 9
12 POLISI DODOMA 9 1 5 3 10 13 8
13 MANYEMA 9 0 7 2 3 6 7
14 PAN AFRICA 9 0 5 4 6 12 5


Hebu tusikie kutoka kwenu juu ya mpambano huu wa kesho. Kazi kwenu wadau

1 comment:

Anonymous said...

Nasikia harufu ya ushindi!!!!!! Naona kuna kila dalili ya kuwachapa. Taarifa nilizozinasa zinaonyesha kuwa Simba wamechanganyikiwa, na toka jana wanatafuta mbinu za kuepuka kipigo. The only obstacle kwetu ni huyu Othman Kazi, siku zote huwa hatutendei haki. Akiona tunawazidi huwa ana-balance mchezo ili tutoke draw na yeye asilaumiwe na yeyote. Kitakachotusaidia kesho ni kupiga mashuti ya mbali, kwani tikitaka kuingia kwenye 18 atakuwa ana-frustrate move zetu.