Monday, October 22, 2007

TANGAZO KWA WANAOTAKA UANACHAMA

Uongozi wa Young Africans Sports Club unawatangazia wapenzi wake wote kwamba utaanza kutoa fomu za maombi ya wanachama wapya kuanzia Jumatatu tarehe 22 Oktoba 2007.

Fomu hizo zitapatikana katika Makao Makuu ya Klabu, Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam na kwenye matawi ya Yanga kwa bei nafuu ya 1000/= kwa kila fomu.

Kila mwombaji ahakikishe anapata risiti ya malipo atakayotoa kwa ajili ya fomu.

Maelezo na maelekezo mengine kwa mfano, jinsi ya kujaza fomu hizo, kiasi cha ada na mahali pa kulipia ada zitapatikana kwenye fomu hiyo na kwa wagawaji wa fomu hizo. Tunawaomba msisite kuuliza.

Tunawakaribisha wapenzi wa Yanga kwenye klabu yetu. Imarisha Klabu yako.

Yanga Imara, Daima mbele, Nyuma mwiko.

Imetolewa na uongozi wa Yanga kupitia vyombo mbalimbali vya habari.


3 comments:

Anonymous said...

Asante kwa taarifa hii muhimu.

Lakini mimi swali langu ni lile lile. Wapenzi walio nje ya nchi na wanataka kuwa wanachama wanafanyaje? Kwanini tusitumie teknolojia kuwapata na hao.kwa walio nje ya nchi wangeweza kutumia electronic copy ya form wakajaza na kurudisha (a simple solution).

Nitashukuru kama kiongozi yeyote atasoma hapa na kutueleza utaratibu, kama upo!

JZah

Anonymous said...

Mimi ni mpenzi wa Yanga wa siku nyingi. Naishi Ulaya ya Kaskazini. Ningependa kuwa mwanachama. Je, nifanyeje?

Anonymous said...

Kwa wenye maswali Tafadhali wasiliana na katibu mwenezi kupitia 0787 619988