Wednesday, October 24, 2007

Leo ni leo huko Morogoro

Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na maelfu ya mashabiki wa kandanda imewadia. Leo ni Yanga na Simba uwanjani huko Jamhuri Morogoro.

Timu hizi mbili zinaingia uwanjani katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ambapo msimu huu vigogo hivi viwili vya soka vimeanza kwa kusuasua sana kiasi cha kuachwa kwa tofauti kubwa ya pointi na timu inayoongoza kwenye ligi hiyo - Prisons.

Yanga itapaswa imchunge sana Julius Mrope pamoja na Moses Odhiambo ambao wamekuwa wakiibeba sana timu ya Simba.

Macho ya mashabiki wengi watakojitokeza uwanjani hii leo yataelekezwa kwa washambuliaji wa kigeni wa Yanga Laurent Kabanda, Aime Lukunku pamoja na Maurice Sunguti. Washambuliaji hao ambao wamesajiliwa kwa pesa nyingi wanatarajiwa kuonyesha kile kilichoifanya Yanga kuvuka mipaka ya nchi na kuwaleta Jangwani.

Nisimalize uhondo wote, hebu tusubiri hizo dk90. Lakini ushindi leo ni lazima.

Mambo yakienda vizuri ungana nasi hapa chini katika comments ili tufahamishane kinachoendelea ndani ya mpambano huo.

11 comments:

Anonymous said...

Kila la kheri 'vijana wa Jangwani'. Malizeni uteji wa miaka kadhaa kwa 'mnyama'!

Anonymous said...

mimi langu nawaombea dua vijana wa Jangwani, inshaalah mwenyezi Mungu atatujaalia ushindi tu leo!!!wakati wa ukombozi umefika na leo ni siku yetu!!
Yanga mbele always!!!

Anonymous said...

Yanga leo ni siku ya ushindi, Mwenyezi Mungu atatubariki na kwa nguvu yake leo tunashinda kwa kishindo!
God bless Yanga!!!!

Anonymous said...

Naungana na mume wangu kuwatakia ushindi Yanga, inshaalah Mwenyezi Mungu atawajaalia!!!

Anonymous said...

Dk zilizokwenda hadi sasa ni 20. Henry Joseph wa Simba amepewa red card dk15 baada ya kumfanyia faulo Tom Mourice. Bado ni 0-0

Anonymous said...

Dk30 Ulimboka Mwakingwe anaipatia Simba bao la kwanza

Anonymous said...

oops... tutumie advantage ya upungufu wao kurudisha hilo bao. Ila wachezaji wetu wawe makini maana nao wanaweza kupewa kadi wakati wowote..

Anonymous said...

Ni mapumziko sasa.

Bado tupo nyuma kwa hilo bao moja.

Anonymous said...

Tumelala tena jamani. Mpira umekwisha 1-0

Anonymous said...

ninachoweza kusema ni kuwa tatizo la Yanga ni la timu nzima kwa ujumla wake!Viongozi wamesajili timu vizuri wakasahau kuwa timu haina kocha,wachezaji nao wanatimiziwa kila kitu yet hamna wanachofanya uwanjani,wanachama nao kila mtu kwa maslahi yake wanaleta vurugu zisizo na msingi klabuni.
sikudhani ipo siku nitasema hivi ila mimi niko Mbeya lakini mechi dhidi ya Prisons next week siwezi hudhuria kwani macho yaliyokuwa uwanjani yananiambia timu inacheza madudu matupu!Pamoja na upungufu wao leo uwanjani lakini Simba wametutawala??haingii akilini!!Nadhani haswa uongozi unapaswa kujitazama upya, mambo ya kupeleka kwa kubahatisha ndo yametufikisha hapa tulipo, hakuna cha mchawi wala nini!!
Manji akae pembeni na hela yake, hawa viongozi,wazee na wachezaji wanamtapeli tu bora akafanye shughuli zingine za maendeleo maana Yanga ni gunia la misumari na halibebeki!!!!

Anonymous said...

Victor,

Para yako ya mwisho imenifurahisha sana. Solution sii kutupa gunia la misumari, bali ni kutafuta namna ya kulibeba kwa urahisi...