Thursday, October 25, 2007

Masikitiko!
Kwa huzuni kubwa bado tunaendelea kuwa wateja wa kudumu wa watani wetu wa Simba licha ya wao kucheza pungufu kwa dk 75 za mchezo huo lakini tumeshindwa kufurukuta mbele yao.

Yanga ilikuwa na kila sababu ya kushinda, kwani hakuna kitu ambacho uongozi na wachezaji umekosa katika kujiandaa na mechi hiyo. Tayari mfadhili wa timu hiyo Yusuf Manji alitoa 50M/= kwa ajili ya mechi hiyo.

Kinachoshangaza hapa ni kwamba hata wachezaji wanashindwa ku-deliver licha ya kupewa matakwa yao yote kwa wakati. Labda wanaweza kutoa kisingizio cha kukosa mbinu mpya kutoka kwa kocha. Lakini hii si sababu ya kutosha, hata enzi za Micho bado wachezaji walikuwa hawawajibiki ipasavyo kiasi kwamba kila siku walikuwa wakipewa adhabu za kusimamishwa mara kwa mara.

Mbali ya kufungwa, bado mashabiki wa Yanga waliendelea na fujo walizozianza kabla ya mchezo lakini safari hii waliwageukia wachezaji wao wenyewe na kuanza kuwaangushia kipigo kutokana na kuendeleza uteja kwa Simba. Awali kabla mchezo haujaanza, mashabiki hao walimpiga jiwe usoni mchezaji Haruna Moshi kiasi kwamba alishindwa kuanza mechi hiyo.

Simba hivi sasa wamefikia hatua ya kutamba kwamba mechi ijayo kwa vile wao ndiyo watakuwa wenyeji, wanaomba wachezee kwenye Uwanja wa Kaunda (wa Yanga) ili angalau Yanga waweze kushinda.

Hebu tusikie maoni yenu wadau.

8 comments:

CM said...

(HAYA MAONI YALITOLEWA JANA Oct 24, 2007 6:49:00 PM NA MDAU VICTOR)

ninachoweza kusema ni kuwa tatizo la Yanga ni la timu nzima kwa ujumla wake!Viongozi wamesajili timu vizuri wakasahau kuwa timu haina kocha,wachezaji nao wanatimiziwa kila kitu yet hamna wanachofanya uwanjani,wanachama nao kila mtu kwa maslahi yake wanaleta vurugu zisizo na msingi klabuni.
sikudhani ipo siku nitasema hivi ila mimi niko Mbeya lakini mechi dhidi ya Prisons next week siwezi hudhuria kwani macho yaliyokuwa uwanjani yananiambia timu inacheza madudu matupu!Pamoja na upungufu wao leo uwanjani lakini Simba wametutawala??haingii akilini!!Nadhani haswa uongozi unapaswa kujitazama upya, mambo ya kupeleka kwa kubahatisha ndo yametufikisha hapa tulipo, hakuna cha mchawi wala nini!!
Manji akae pembeni na hela yake, hawa viongozi,wazee na wachezaji wanamtapeli tu bora akafanye shughuli zingine za maendeleo maana Yanga ni gunia la misumari na halibebeki!!!!

Anonymous said...

Nadhani viongozi hawana vision ya ushindi. Wanatazama pesa tu.

Mfano wenzetu wanafanya vikao vya siri vya wapenzi hasa wa club (friends of simba) na kupanga wafanye nini ili washinde.

Waliona Chuji anakuja vizuri wakamfungia tena miezi mitatu kwa madai eti makosa yake yamekuwa yakijurudia. Ebu jiulize chuji amewahi kupewa adhabu ya utovu wa nidhamu lini mpaka isemekane anarudia. UONGOZI UKAKAA KIMYAAAA

wakajua Ivo ni mgonjwa, chove ni bomu, wakamfungia Haule mechi 6.UONGOZI UKAKAA KIMYAAAA MAANA MWENYEKIT WETU NI TFF PIA

Wakaangalia goal getter pale ni Mwalala peke yake. Refa akamchokoza naye akamtukana akafungiwa. UONGOZI UKAKAA KIMYAAAA MAANA WALIKUWA BUSY NA MIL 50 ZA MANJI

Sasa niambie utashinda namna gani?
Kama ningekuwa ni mimi ningetishia kutopeleka timu uwanjani kama wachezaji hawatafunguliwa kama mbinu za kuondoa concentration ya mechi, na kimya kimya ningejiandaa. Lakini viongozi wetu mbinu hakuna.

Usajili wa wachezaji ni mkorogo mtupu. Mimi kuna mchezaji nilitumia gharama zangu binafsi kuwasiliana nae, kumuandaa na akaonyesha mwelekeo. Nikamwambia mwenyekiti. Bei yake 30,000 USD. Nikaambiwa huyo ni ghali mno. Cha ajabu wakaletwa hao wengine bei kubwa zaidi uwezo hakuna.

Mwisho, Yanga pale kuna wachezaji uwezo ni mdogo. Na sasa kilichobaki ni kuwaroga wenziwe tu lakini hawafukuzwi. Yanga haiitaji 30players huku kumi wakiwa hawana lolote. FUKUZA

Mkumbukeni Marehemu TAMBWE LEYA. machozi yananitoka......

VIONGOZI NI BOMU SANA. KWA NINI WANAJUA HATUNA KOCHA WASITAFUTE KOCHA WA MUDA MZALENDO MWENYE UWEZO? MBONA SIMBA HUWA WANAFANYA HILO TENA KWA UMAKINI NA INAWASIDIA? HIZO MILIONI 50 ZA MANJI KUMI TUU ZINGETOSHA KUMPATA KOCHA MZURI WA HAPAHAPA MUDA MREFU ULIOPITA AKAANDAA TEAM VIZURI. CHAMANGWANA ALISHAONESHA KUWA HAWEZI KUWA NA MBINU MPYA TENA. WATU KILA SIKU WANARUDIA MAKOSA YALEYALE!! UJINGA UMEZIDI KWA SABABU YA MASLAHI BINAFSI.

MZOZAJI

Anonymous said...

Yes, nadhani viongozi wanastahili lawama nyingi/zote kwa koboronga kwa timu, sio tu kwenye mchezo wa jana bali ligi yote hadi sasa.

Tangu wamengia madarakani hawajaonesha kufanya mikakati yoyote ya kuendeleza timu. Mambo yanakwenda yenyewe tuu. Tukibahatisha kushinda mechi, wanavimba vichwa wakati wanajua hakuna lolote walilofanya kuleta ushindi huo.

Timu ilianza kubadilika kiuchezaji wakati wa Micho, akakosa ushirikiano aliokuwa akiupata wakati wa kina Kifukwe na wenzake akaamua kujiondoa. Viongozi nao wamekaa miezi minne yote bila hata kifikiria kupata replacement yake!

Hapo ndo nasema kuwa tutaendelea kufukuza kiongozi huyu na kuweka yule maisha yetu yote, lakini solution ya kudumu ni kuiweka timu mikononi mwa watu watakaoiendesha professionally, na viongozi wetu waendelee na mambo yao ...

Anonymous said...

The only solution is to chase these leaders away!! hatuna njia nyingine ila kuwafukuza hawa mamluki wa Simba,kwanza ni ajabu kuwa na kiongozi ambaye ni kiongozi wa TFF aongoze Yanga tangu klabu hii ianzishwe.Ni kama vile Mw.kiti wa Chadema awe waziri katika serikali ya CCM halafu wakishakaa kwenye kikao cha baraza la mawaziri na wakapitisha hoja ya kuwaangamiza wapinzani,unatarajia huyu kiongozi wa Chadema aliyeko serikalini aigeuke serikali?? Ni aheri Yanga iongozwe na wazee kama kina Jabir Katundu na Yusuph Mzimba kuliko kuongozwa na vibaraka wa Simba walioingia kwa mgongo wa TFF madarakani.Enyi wanachama wa Yanga mko wapi?? hamuoni aibu kufungwa na Simba kila siku?? hamuoni aibu kuwa mkiani kwenye ligi?? Enyi mashabiki wa Yanga,wapenzi na wanachama wa Yanga ni lini mtachagua viongozi wa kweli ambao ni wanachama damu wa Yanga?? ni lini aibu hii ya kutukanwa matusi na Simba itakwisha?? Lini mtawaenzi kwa vitendo wazee wetu wlioiongoza Yanga kwa mafanikio?? ni lini mtafuata mfano wa akina Mangara,Mpondela,Tarimba,Kifukwe na wengineo..macho kwenu wana-yanga vinginevyo mtafungwa hata miaka 10 mfulilizo na Simba....Siwezi kuwa Adui kwa kusema ukweli...

Anonymous said...

1. Vipi kuhusu yale magoli ma 3 inayosemekana refa kayakataa? Kuna ukweli wowote au ni visingizio tuu?

Wengine tuko mbali hatukubahatika kuona huo mpira.

-----------------

2. Nadhani tumefungwa hii mechi na zingine zilizopita kwa vile uongozi hauko pamoja. Siamini kama mgogoro wa mkiti na Katibu umeisha kabisa na wanakaa na kupanga mikakati ya pamoja. Sasa bila mipango ya pamoja unategemea timu itashindaje?

Timu alokuwa nayo Micho kwenye ligi ndogo ilikuwa nzuri, hata tulipofungwa mchezo wa mwisho kwa penalty watu wote tulielewa kuwa ni bahati mbaya. Sasa tumeongeza wachezaji 5 wa kimataifa, tunashindwaje kuwafunga hata timu iliyo mkiani?

PENDEKEZO:
Tayari tumechemsha hii round ya kwanza. Round ya pili, timu iwekwe kambini nje ya Dar au Moro (napendekeza Mwanza au Tabora), chini ya makocha wapya. Timu ibadilishwe kimfumo, na lengo liwe kushinda mechi zote za second round.

Kama inawezekana, timu iwe chini ya kamati maalum, itakayofuatilia maendeleo yake on daily basis, badala ya viongozi ambao inaelekea wako mbali na slow kiutendaji.

Anonymous said...

Kwa uongozi wa huyu Madenga hatuwezi kwenda kama pesa imetolewa iankuwaje hata Hotelini washindwe kulipia? sasa hela zote mil 50 zimekwenda wapi?