Friday, October 05, 2007

Mtihani wa kwanza wa Chamangwana

Jack Lloyd Chamangwana kesho anakabiliwa na mtihani wake wa kwanza tangu akabidhiwe kwa muda mikoba ya kuinoa Yanga katika ligi kuu ya Vodacom pale klabu hiyo itakapopambana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Yanga inatakiwa ishinde mechi hiyo ili ijiweke pazuri katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaongozwa na Prisons ya Mbeya ambayo imeshinda mechi zote. Prisons ina pointi 12 wakati Yanga ina pointi 3 tu katika michezo minne.

Vipigo tulivyopata hadi sasa vinatosha, kinachotulinda hadi sasa ni kule kufanya vibaya kwa watani zetu Simba ndiyo maana tunavichukulia vipigo hivi kama 'bahati mbaya'. Hii imeingia sana katika mawazo ya mashabiki walio wengi lakini tukiangalia hali halisi ni kwamba tayari tumeachwa pointi 9 na timu inayoongoza ligi hiyo.

Tunaitakia kila la heri vijana wetu ambao kwa muda tutawaita 'Jack Boyz' katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

(Msikose kucheki updates za game yetu inavyoendelea ndani ya dk90 kwa kuangalia hapa chini katika comments)

5 comments:

Anonymous said...

Tumepata bao ktk ya 17

Anonymous said...

Afadhali maana viroho vilikuwa vinadunda. Mambo yaendelee hivyo hivyo.

Anonymous said...

Mpira umekwisha. Tumeshinda 1-0, bao limefungwa na Abdi Kassim "Babi"

Anonymous said...

Wow, afadhali... wembe uwe huu huu.

Hongereni vijana na viongozi.

CM said...

(Usahihi) Goli la Yanga limefungwa na Maurice Sunguti baada ya kupata pasi kutoka kwa Abdi Kassim.