Monday, October 15, 2007

Sare na Mtibwa Sugar

Yanga jana ilitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri huko Morogoro.

Wafungaji wa mabao hayo walikuwa Mecky Mexime - Mtibwa katika dk 4 huku lile la Yanga likisawazishwa na Hussein Sued dk 49.

Katika mchezo huo, Yanga ilimpoteza mshambuliaji wake Ben Mwalala baada ya kupewa kadi nyekundu katika dk ya 61 ya mchezo.

Yanga sasa imefikisha pointi 10.


No comments: