Monday, October 29, 2007

Wanne kuadhibiwa Yanga?

Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa na Amir Maftah

Wachezaji wanne wa Yanga Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah pamoja na Ben Mwalala huenda wakakabiliwa na adhabu kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo, kufuatia kutoweka kwao kambini mara baada ya mechi dhidi ya Simba.

Wachezaji hao walitoweka kambini kwa madai kwamba wameshindwa kuvumilia tuhuma wanazopewa kwamba wameihujumu timu hiyo katika mchezo dhidi ya Simba. Baadhi ya wachezaji wamekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema kwamba hawataki kuichezea tena Yanga kutokana na tuhuma hizo.


Kabla ya mechi hiyo, uongozi wa klabu hiyo ulimsimamisha mchezaji mwingine Edwin Mukenya kwa kukosekana kwake kambini mara kwa mara.


Kufuatia kukosekana kwa Ivo Mapunda, Yanga sasa imebakiwa na kipa mmoja tu - Jackson Chove ambaye alidaka jana katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu. Kipa mwingine wa Yanga Ben Haule amesimamishwa mechi sita na TFF kwa utovu wa nidhamu uwanjani.

Hivi karibuni wachezaji hao wataitwa na Kamati Kuu ya klabu hiyo ili wajielezee kuhusu kutoweka kwao kambini.


No comments: