Monday, October 29, 2007

Ahueni yapatikana Arusha

Maurice Sunguti

Yanga jana ilipata ahueni katika ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa timu ya JKT Ruvu 1-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Shiekh Amri Abeid huko Arusha.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji kutoka Kenya Maurice Sunguti katika dakika ya 12 ya mchezo. Yanga jana haikuwatumia wachezaji wake Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa na Amir Maftah kutokana na wachezaji hao kutakiwa na Kamati Kuu ya klabu kutoa maelezo ya kitendo chao cha kutoroka kambini baada ya uliopita mchezo dhidi ya Simba.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa imejikusanyia pointi 15 katika michezo 11 iliyocheza hadi sasa.

No comments: