Wednesday, October 03, 2007

Yanga uwanjani tena leo


Ligi Kuu ya Vodacom leo inaingia mzunguko wake wa nne kwa timu ya Yanga kuingia katika uwanja wa Jamhuri huko Morogoro kupambana na timu ngumu ya Polisi Morogoro.

Maafande hao wa Moro ambayo hadi hivi sasa ina pointi 5, ni moja ya timu ngumu kufungika hasa inapokutana na vigogo vya soka nchini. Ikiwa chini ya kocha John Simkoko na mshambuliaji wao hatari Mjarubi Julius leo wanatarajia kutoa upinzani mkali kwa vijana wa Jangwani.

Yanga leo itawakosa majeruhi Yusuf Hamis, Thomas Mourice, James Chilapondwa na Said Maulid. Aidha hati ya uhamisho wa kimataifa ya Ben Mwalala bado haijafika nchini kutoka huko Malaysia hivyo ataendelea kukaa nje.


Yote juu ya yote dua zetu zinaelekezwa huko Morogoro, pointi 3 ni muhimu sana kwetu.


Kwa wale watakaopenda kupata kile kinachoendelea huko Moro ndani ya dk 90 wanaweza kucheki comments hapo chini - tutafahamishana kadri mabao yatakavyokuwa yanaingia.
Mungu Ibariki Yanga.

6 comments:

Anonymous said...

Kila la kheri vijana. Tumeshaondoa nuksi sasa hivi ni kukandamiza tu.

Anonymous said...

Fikiri Hussein anaipatia Polisi Moro bao ktk dk ya 52.

Anonymous said...

Tumebakiwa na points zetu 3 katika mechi 4. Nafikiri mmenielewa.

Anonymous said...

Mimi sijui hata niseme nini

Na hao wenzetu?

Anonymous said...

Kwa wale walioshindwa kuelewa, leo tumefungwa 1-0.
Uongozi wa Yanga umemrejesha kwa muda Jack Chamangwana baada ya vipigo kuendelea kurindima Jangwani.

Simba wametoka sare 0-0 na Manyema.

Mengi zaidi kesho.

CM

Anonymous said...

Its so sad. Hivi ni tunafungwa kiufundi tuu ama kuna kitu kingine.? Maana haiingii akilini, Yanga kufungwa na vitimu vidogo kama hivi!