Yanga uwanjani tena leo
Ligi Kuu ya Vodacom leo inaingia mzunguko wake wa nne kwa timu ya Yanga kuingia katika uwanja wa Jamhuri huko Morogoro kupambana na timu ngumu ya Polisi Morogoro.
Maafande hao wa Moro ambayo hadi hivi sasa ina pointi 5, ni moja ya timu ngumu kufungika hasa inapokutana na vigogo vya soka nchini. Ikiwa chini ya kocha John Simkoko na mshambuliaji wao hatari Mjarubi Julius leo wanatarajia kutoa upinzani mkali kwa vijana wa Jangwani.
Yanga leo itawakosa majeruhi Yusuf Hamis, Thomas Mourice, James Chilapondwa na Said Maulid. Aidha hati ya uhamisho wa kimataifa ya Ben Mwalala bado haijafika nchini kutoka huko Malaysia hivyo ataendelea kukaa nje.
Yote juu ya yote dua zetu zinaelekezwa huko Morogoro, pointi 3 ni muhimu sana kwetu.
Kwa wale watakaopenda kupata kile kinachoendelea huko Moro ndani ya dk 90 wanaweza kucheki comments hapo chini - tutafahamishana kadri mabao yatakavyokuwa yanaingia. Mungu Ibariki Yanga.

6 comments:
Kila la kheri vijana. Tumeshaondoa nuksi sasa hivi ni kukandamiza tu.
Fikiri Hussein anaipatia Polisi Moro bao ktk dk ya 52.
Tumebakiwa na points zetu 3 katika mechi 4. Nafikiri mmenielewa.
Mimi sijui hata niseme nini
Na hao wenzetu?
Kwa wale walioshindwa kuelewa, leo tumefungwa 1-0.
Uongozi wa Yanga umemrejesha kwa muda Jack Chamangwana baada ya vipigo kuendelea kurindima Jangwani.
Simba wametoka sare 0-0 na Manyema.
Mengi zaidi kesho.
CM
Its so sad. Hivi ni tunafungwa kiufundi tuu ama kuna kitu kingine.? Maana haiingii akilini, Yanga kufungwa na vitimu vidogo kama hivi!
Post a Comment