Friday, November 09, 2007

Amir Maftah atadumu K'njaro Stars?
Mchezaji pekee wa Yanga Amiri Maftah ni miongoni mwa wachezaji 19 walioripoti kwa ajili ya mazoezi katika timu ya Taifa ya Tanzania Bara - Kilimanjaro Stars.

Uwepo wa Maftah katika kikosi hicho upo katika hatihati kwani uongozi wa Yanga huenda ukamwita ili atoe maelezo juu ya kutoroka kwake kambini mara baada ya mchezo kati ya Simba na Yanga.

Ikumbukwe kwamba mchezaji huyo pamoja na wenzake Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa na Ben Mwalala walitoroka kambini mara baada ya mchezo huo na baada ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu, Ivo na Nsajigwa walifungiwa miezi sita wakati Mwalala alipewa onyo kali. Maftah hakujieleza mbele ya Kamati hiyo kwa vile alikuwa nje ya Dar es Salaam, hivyo aliwekwa kiporo hadi hapo atakapoitwa tena.

Endapo mchezaji huyo atafungiwa na kamati kuu halafu TFF ikiidhinisha adhabu hiyo, basi huo ndiyo utakuwa mwisho wa Maftah katika kikosi hicho.

Tukae chonjo.


2 comments:

World of Soccer said...

Guys kama mwanamichezo kuona mchezaji akifungiwa inauma na wakati mwingine mtu kuvunjika moyo. Lakini ningependa tutambue kuwa katika hali yoyote nidhamu kwa mchezaji ni kitu muhimu,haijalishi mazingira lakini nidhamu ni silaha ya mchezaji kwa maendeleo yake mwenyewe na klabu yake.

Hasara za utovu wa nidhamu zinakwenda pande zote lakini hasara ni kubwa zaidi kwa mchezaji kuliko klabu. Klabu inauwezo wa kupata mchezaji mwingine tena anayeweza kuwa bora kuliko wa kwanza.

Na moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikituumiza watanzania ni nidhamu ya wachezaji. Nidhamu kwa viongozi na walimu, nidhamu ya mazoezi (Kwa ratiba ya mazoezi ya timu hata ratiba binafsi ya mazoezi).

Lakini hili jambo halianzii hapa, sababu zake zinakwenda mbali hadi maandalizi ya awali ya mchezaji toka alipokuwa mdogo. kuna vijana waliokosa huduma nzuri toka majumbani mwao na timu zao za awali hadi kupelekea kuwa na tatizo ambalo kitaalam linajulikana kama Attention deficit disorder.

I stand to be corrected. Tembelea blogu yangu www.tuntucoach.blogspot.com

Regards

Tuntufye

Anonymous said...

Kwa vile uongozi umeshatoa somo kwa wachezaji wote kupitia kwa Nsajigwa na Ivo, nadhani Amir aitwe na kupewa onyo tuu, basi sio kufungiwa. Nadhani hili ni kosa lake la kwanza akiwa Yanga.

Bila shaka atakuwa ameshaona kosa lake, kwa hiyo aachwe aendeleze kipaji chake, na viongozi wa-concentrate kuandaa timu for next year. Yaliyopita yamepita