Monday, November 26, 2007

Mukenya kuuzwa Simba?Edwin Mukenya

Kuna habari kwamba Yanga ipo tayari kumuachia mchezaji wake wa kimataifa kutoka Kenya Edwin Mukenya kwa klabu yeyote itakayomhitaji.

Akizungumza na redio moja jijini Dar es Salaam jana usiku, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Imani Madega amezitaka klabu zinazotaka kuchukua wachezaji wa Yanga kufanya kwanza mazungumzo na uongozi badala ya kuingia mkataba na mchezaji bila kupata uhakika wa uhalali wa mchezaji huyo kuhama Yanga.

Wiki chache zilizopita, baadhi ya wachezaji wa Yanga wamekuwa wakihusishwa na kuhama klabu hiyo. Inasemekana Edwin Mukenya ana mpango wa kuhamia Simba wakati wachezaji Thomas Mourice na Amri Kiemba walihusishwa na kuhamia Miembeni ya Zanzibar.

2 comments:

Anonymous said...

Kuuzwa kwa Mukenya ni kosa kubwa.Hakuna timu inayouuza mchezaji wake muhimu bila kusikiliza mahitaji ya mchezaji,Mukenya ameuuzwa kwa kudai haki yake.Wachezaji wa kutoka Kongo na Mwalala wamepewa pesa nyingi kusajili na huku hakuna cha maana walichoifanyia timu yetu mpaka sasa.Viongozi waache chuki na wachezaji wanaodai haki yao.Ndio maana Thomas na Kiemba wamekimbilia Miembeni.Kama ni suala la kutomlazimisha mchezaji mbona Ivo tupo nae na inajulikana wazi anapenda timu tuliyo na upinzani nae tokea akiwa shule????

Anonymous said...

Nilisema kwenye comment yangu hapo juu na ushahidi wa Mukenya kwa kauli yake mwenyewe umethibitisha kwamba sikuwa nasema uongo.Wapo wengi tuu wachezaji wa namna hiyo ndio maana hatuiishi kufungwa na Simba kila mra.Viongozi wabovu wanaomsujudia Mfadhili asiye na mbele wala nyuma kuhusu uongozi wa mpira.Bado tuna kazi kubwa hta tuwe na makocha wazuri watachoka kama alivyochoka Micho,Wewe unasomea wachezaji Al Badir siku ya mchezo na vitisho kwamba atakayekwenda kinyume atakufa unategemea watakuwa fit kisaikolojia???Halafu viongozi hao wanadai kuwa ni wasomi.Usomi sio vyeti tu bali matendo.Inatia uchungu sana.Katika wachezaji wa viungo wazuri tuliowakosa Mukenya ni muhimu.Tulikazaniz kubaki na Athumani Idi lakini limekuwa kosa kubwa kwani mpira wake umeshuka sana ndio maana amebakia kufanya fujo tu kila mara huku akilindwa na kukumbatiwa na viongozi.