Wednesday, November 28, 2007

Umepima? Ingia kambini

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa soka la Tanzania, wachezaji wa Yanga wametakiwa kupimwa kwanza afya zao ndipo waende kambini huko Mwanza.

Mkakati huu ni miongoni mwa mambo mapya kutoka kwa kocha mpya kutoka Serbia, Dusan Kondic, ambaye anasaidiwa na daktari na kocha wa viungo, Spaso Sokolovski katika kuinoa klabu ya Yanga.

Inasemekana makocha hao wanataka rekodi za afya za wachezaji wote kabla ya kuingia kambini kuanzia kesho huko Mwanza. Aidha wale watakaochelewa kupimwa wakiwa Dar es Salaam watalazimika kupimwa afya zao huko huko Mwanza kabla ya kuanza kambi ya mazoezi.

Mambo mapya haya kwa vilabu vyetu.

5 comments:

Anonymous said...

Hayo ndio mambo ya maendeleo. Safi sana Kondik.

Anonymous said...

Kuna hii habari kuhusu kocha mkuu wetu imenifurahisha sana. Naomba wanachama na wapenzi tuwape ushirikiano makocha wetu. Wana mwelekeo mzuri wa maendeleo.

http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=3169

Wadau wengine mnasemaje?

JZah

MOSONGA said...

Kiutaratibu wachezaji wanatakiwa kupimwa afya zao wakati wa kusajiliwa.
Mchezaji hawezi kupewa mkataba kama hatafaulu zoezi la kupima afya (medical).
Sasa kama wameshasajiliwa na kupewa mkataba, unapowapima kabla ya kwenda kambini unataka upate nini (lengo ni nini!!).
Kama ni suala la match fitness ni mambo ya ndani klabuni wala haihitaji uwatangazie wapime.
Halafu anapotangaza wapime anamaanisha waende Muhimbili au ...
Klabu inatakiwa kuwa na facility hizo na mambo yanafanyika ndani kwa ndani klabuni!!

Anonymous said...

Utaratibu huo ni mgeni kwa timu za Tanzania. Hakuna mchezaji anayepimwa afya kabla ya kusajiliwa Tanzania. Sasa nadhani ilibidi itangazwe ili hata wachezaji wenyewe na wapenzi wajue maana ya zoezi hilo. Nadhani next time hakutakuwa na matangazo, maana kila mtu atakuwa anajua ndio utaratibu uliyo!

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___