Thursday, November 29, 2007

Yanga wakubaliana na Miembeni
Amri Kiemba - Kuhamia Miembeni

Klabu ya Yanga imekubaliana na mabingwa wa soka wa Zanzibar Miembeni kuhusu uhamisho wa wachezaji wake wawili Amri Kiemba na Thomas Mourice.

Katibu Mkuu wa Yanga Lucas Kisasa amesema uongozi wa klabu ya Miembeni ulifika klabuni hapo kuonana nao kwa ajili ya uhamisho wa wachezaji hao na tayari wamefikia muafaka. Kisasa amewashukuru uongozi wa klabu ya Miembeni kwa kufuata utaratibu na kuongeza kwamba uongozi wa Yanga hawana nia ya kuwang'ang'ania wachezaji waendelee kuichezea klabu hiyo.

Akizungumzia suala la Edwin Mukenya, Kisasa amesema uongozi wa klabu inayotaka kumsajili kiungo/beki huyo ufike klabuni hapo kufanya mazungumzo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho wa mchezaji huyo. Inasemekana Simba ipo mbioni kumsajili Mukenya lakini hadi sasa haijatia mguu Jangwani kushughulikia suala hilo.

Kuhusu suala la Said Maulid 'SMG', Yanga bado inasubiri majibu kutoka katika klabu ya Bravo Marquiz ya Angola kuhusu suala lake la uhamisho.

No comments: