Wednesday, November 14, 2007

Zoezi la wanachama wapya:

Ndugu wadau, kwa siku za hivi karibuni yale yanayojiri katika klabu yetu si mengi sana kwa hiyo si vibaya tukibadilishana mawazo kuhusu zoezi zima la wanachama wapya.

  • Fomu zilianza kutolewa kwenye matawi ya klabu ya Yanga tangu Oktoba 21 mwaka huu na katika fomu hizo mwombaji anatakiwa ajaze na kisha kuzirejesha tawini hapo ikiambatanishwa na picha tatu za passport size. Fomu moja iliuzwa kwa 1000/=.
  • Baada ya hapo fomu hizo zitapelekwa makao makuu ambako zoezi la kuhakiki fomu hizo litafanyika na majina ya wanachama waliokubaliwa maombi yao yatadhihirishwa. (Zoezi hili lilipangwa kuanza leo)
  • Kama jina lako limepitishwa, unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye benki ya CRDB kulipia ada ya uanachama (12,000/= kwa mwaka) pamoja na gharama ya kadi(2000/=) kupitia akaunti namba 01J095095800 yenye jina la Young Africans Sports Club na si kwa viongozi wa matawi.
  • Baada ya kulipa kwenye akaunti hiyo, mwanachama anatakiwa kupeleka hati ya malipo (pay slip) katika tawi ili kuthibitisha kuwa tayari amelipa na kisha anapatiwa kadi yake ya uanachama.
Sijui wadau mnaonaje kuhusu hili zoezi linaloendelea?


4 comments:

Anonymous said...

Utaratibu ukoje kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga walioko nje ya nchi (mfano Ulaya na Marekani).
Tunaomba ufafanuzi au tamko rasmi kutoka uongozi wa Yanga kuhusiana na hili.
(au mwanachama lazima awe anaishi nchini tu?)

Anonymous said...

Kwenye forms za uanachama kuna namba ya simu kwa ajili ya mawasiliano zaidi kwa hiyo bila shaka mlio nje ya nchi mtaweza kupiga simu na kupewa ufafanuzi zaidi.

Namba hiyo ni +255 732203757

Au pia mnaweza kuwasiliana na Katibu Mwenezi ili kusikia kauli ya viongozi(+255 787 619988)

Anonymous said...

Naomba atakayepiga na kupewa jibu asisite kuliweka hapa ili wote tunufaike.

Anonymous said...

O.K. Thanks.