Wednesday, December 05, 2007

Mwalala, Chuji, Haule huru
Ben Haule - amekosa mechi 5

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la soka nchini TFF imewaachia huru wachezaji watatu wa Yanga Ben Mwalala, Ben Haule na Athumani Iddi.

Kamati hiyo ya Nidhamu ya TFF imetengua uamuzi wa awali uliokuwa umetolewa na Kamati ya Mashindano ya TFF kwa wachezaji hao baada ya Yanga kuwakata rufaa. Kamati ya Nidhamu imedai kwamba wachezaji hao wamefungiwa bila ya kuitwa kutoa utetezi wao kabla ya kuhukumiwa.

Wachezaji hao ambao walifungiwa na Kamati ya Mashindano ya TFF, walikuwa wakikabiliwa na adhabu mbalimbali za makosa ya utovu wa nidhamu.

Athumani Iddi alituhumiwa kumtukana mwamuzi wa mchezo dhidi ya Coastal Union huko Tanga na akafungiwa miezi 3. Ben Mwalala alituhumiwa kumtukana mwamuzi katika mchezo kati ya Yanga na Mtibwa huko Morogoro na akafungiwa kucheza mechi 6. Ben Haule alituhumiwa kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Toto Africa na akafungiwa mechi 6.

Hata hivyo uamuzi huo umechelewa sana kwani tayari Mwalala na Haule wameshakosa mechi 5 ilihali Athumani Iddi alitarajiwa kumaliza adhabu yake mwisho wa mwezi huu.

Soka la Bongo hilo.

2 comments:

Anonymous said...

Justice delayed is justice denied!

Anonymous said...

Makosa mengine TFF wangekuwa wanatoza faini wachezaji badala ya kuwafungia muda mrefu -hii inaua maendeleo ya ukuaji vipaji vya wachezaji na inaathiri mipango ya Timu ya Taifa! Adhabu kama hizi hazitolewi kama funzo bali kukomoana tu!!!!
-Mosonga