Thursday, January 17, 2008

Kondic: Yanga kaaazi kweli kweli

Kocha Mkuu wa Yanga Dusan Kondic amesema anakabiliwa na matatizo katika ufundishaji wake kutokana na wachezaji kutokuwa na elimu.

Akizungumza Jijini Dar jana, Kondic amesema elimu ndog waliyonayo wachezaji wa Yanga ndicho kitu kinamkwamisha kufanya kazi yake kwa ufasaha na kusababisha wachezaji wasielewe mafunzo yake.

Alisema wachezaji wengi wana uelewa mdogo hali ambayo ni hatari kwa maendeleo ya mpira.

Kondic alisema licha ya elimu, wachezaji hao wanaonekana hawakupata mafunzo ya mpira wa miguu katika ngazi ya wawli hivyo kufanya kazi yake iwe kama anaanza upya kuwafundisha soka.

Alisema baada ya miezi 6 atakuwa amewasoma vizuri wachezaji hao, ili kujua nani anastahili kuendelea kubaki katika kikosi hicho.

Miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja anaitwa Kaduguda aliwahi kusema mambo kama haya kwa timu ya Taifa, akashambuliwa kwa maneno. Sasa maneno yale yale yamerudiwa na mtu mwingine, tena wa nje. Tunasubiri kusikia kutoka kwenu.

3 comments:

Anonymous said...

Kwani uongo.Kiwango hakirdhishi licha ya kufundishwa.

Anonymous said...

Elimu ni muhimu sana ktk jambo lolote. Hata kuelewa tuu mambo ya kawaida kunahitaji elimu kiasi fulani. Hiyo ndio sababu hatuna mchezaji wa maana Ulaya (UK, Germany, Italy, Spain, etc). Hata wakienda na mchezaji akawa mzuri, response kwa maelekezo (ambayo inatokana na elimu aliyonayo) inakuwa ndogo.

Pendekezo:
Kocha aendelee nao huku timu za watoto zikipewa umuhimu unaotakiwa. Hizo ndio zitatoa aina ya wachezaji anaowataka. Kocha pia awe na session na timu za vijana, awapike anavyotaka.

Hata Maximo ingawa hajalalamika (sababu ya kuogopa kuharibu PR yake) naye anakabiliwa na tatizo hilo, ndo maana kila siku anabadili wachezaji, bila mafanikio.

Anonymous said...

Kondíc pasua kichwa hana lolote.Nimekwenda kwenye mazoezi wachezaji wanakimbizwa tu na kuruka viunzi.Hamna mbinu za uchezaji wala formation yeyote inayochezwa bora liende.