Thursday, January 31, 2008

Mwalala na Maftah hawana makosa!
Ben Mwalala (kushoto) na Amir Maftah(kulia)

Hatimaye wachezaji wawili wa Yanga, Ben Mwalala na Amir Maftah wamefahamu hatma zao baada ya kamati ya nidhamu ya timu hiyo kuwaachia huru kwa vile hawakuwa na makosa.

Awali, nyota hao walikuwa wasimamishwe pamoja na Shadrack Nsajigwa na Ivo Mapunda kwa madai ya utovu wa nidhamu wakati timu hiyo ikiwa kambini Morogoro.

Oktoba 25, mwaka jana, siku moja baada ya kufungwa na Simba, Mwalala, Maftaha, Nsajigwa na Ivo waliondoka kambini bila ruhusa ya uongozi.

Hata hivyo, uongozi wa Yanga uliwafungia Nsajigwa na Ivo huku ikiwaacha Mwalala na Maftah kutokana na nyota hao kujitetea walikuwa na matatizo.

Mwalala, aliyekuwa amefungiwa kwa miezi mitatu kwa kipindi hicho, alijitetea kwenda kwao Kenya kwa matatizo ya kifamilia kama ilivyokuwa kwa Maftah.

Baada ya Kamati Kuu ya Yanga kuwafungia Nsajigwa na Ivo kwa miezi sita, Maftah na Mwalala wakawekwa kiporo, lakini imebainika nyota hao hawana kosa.

Akizungumza katika makao makuu ya klabu hiyo iliyopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam, jana, Katibu Mwenezi wa Klabu hiyo, Francis Lucas, alisema huo ni uamuzi uliofikiwa Januari 25.

Kuhusu Maftah ilibainika kuwa aliomba ruhusa kwa aliyekuwa kocha msaidizi, Razak Siwa, kutokana na kuuguliwa na mama yake jijini Mwanza.

Mwalala naye aliomba ruhusa kwa Kocha Dusan Kondic, ya kwenda kwao Kenya ingawa alishindwa kurejea kwa muda uliotakiwa.

Pamoja na kuwasamehe, kamati imewapa onyo kali nyota hao kwa kushindwa kuwasilisha taarifa zao mapema.

Hii imekaaje wadau, naona kama akina Ivo hawajatendewa haki!

4 comments:

Anonymous said...

heri waende simba.

Anonymous said...

Well, wamesema kama Ivo na Shadrak wanataka kucheza, wahame. Kwa ufupi, hawahitajiki Yanga tena. Sipingi uamuzi huu maana viongoi ndio tumewapa madaraka wafanye maamuzi kwa niaba yetu wengi, lakini naamini tutam-miss Nsajigwa.

Alikuwa anajituma sana, na kwa vile nadhani hili ni kosa lake la kwanza, angesamehewa, unless yeye amesema hana nia tena ya kuchezea Yanga.

Haya tungalie yajayo, ya kina Ivo ndio yameishia hapo!

Anonymous said...

Ivo kwanza ni Simba damu tokea anasoma.Hilo sio siri.Tusikurupuke kusajili wachezaji wanaopenda timu zingine na hawawezi kuwa professionals na kuichezea Yanga kwa moyo mmoja.

Anonymous said...

Jamani tuache ushabiki, tuwachie viongozi wafanye kazi yao, hili litakuwa fundisho kwa wengine kuwa nidhamu ni ya muhimu.