Friday, January 18, 2008

Tunavunjwa moyo na kocha - Wachezaji

BAADHI ya wachezaji wa Yanga ya Dar es Salaam wamedai hatua ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mserbia Dusan Kondic kusema wachezaji wake wengi hawana elimu si sahihi na inawavunja moyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wachezaji hao walisema Kondic alikosea kutoa kauli hiyo na atawapa wapinzani wa Yanga nafasi ya kuwatania.

"Yeye anaweza kuona ni jambo rahisi, lakini kwa kweli lina matatizo, tutataniwa sana, ilikuwa hakuna haja ya kuzungumza katika vyombo vya habari," alisema mmoja wa wachezaji hao.

Pia mchezaji mwingine alitaja majina ya wachezaji kadhaa aliodai wamefika kidato cha sita na kusema kuwa elimu anayoitaka kocha huyo hawaelewi ni ya aina gani.

"Kocha ni profesa au anataka na sisi tuwe hivyo? Hapa ni Afrika kuna tofauti kubwa sana, lakini elimu haichezi mpira, yeye afundishe soka kashaanza mambo ya kiswahili," alisema mchezaji mwingine.

Alisema umefika wakati kwa uongozi kuangalia maneno anayotamka kocha huyo, ili yasije kuharibu ari ya wachezaji na kujiona si mali kitu.

Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa jana kuhusiana na madai hayo alisema kocha huyo anaelewa anachokizungumza na kwamba uongozi utampa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha Yanga inasonga mbele.

"Mwalimu anajua anachokizungumza, hakuna tatizo, vijana wanahitaji kumuelewa," alisema Lucas.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, kocha huyo alisema kigezo cha elimu ndio sababu kubwa inayomfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi, hali ambayo inamfanya aonekane haeleweki katika mafundisho yake.

Alisema licha ya elimu wachezaji wake wanaonekana hawakupata mafunzo ya mchezo wa mpira wa miguu katika ngazi ya awali na kusema kama viongozi wa timu hiyo wataendelea kuchukua wachezaji wa namna hiyo hakuna kocha watakayemuelewa.

MAJIRA

3 comments:

Anonymous said...

Jana nilitoa maoni haya:
-----------
Elimu ni muhimu sana ktk jambo lolote. Hata kuelewa tuu mambo ya kawaida kunahitaji elimu kiasi fulani. Hiyo ndio sababu hatuna mchezaji wa maana Ulaya (UK, Germany, Italy, Spain, etc). Hata wakienda na mchezaji akawa mzuri, response kwa maelekezo (ambayo inatokana na elimu aliyonayo) inakuwa ndogo.

Pendekezo:
Kocha aendelee nao huku timu za watoto zikipewa umuhimu unaotakiwa. Hizo ndio zitatoa aina ya wachezaji anaowataka. Kocha pia awe na session na timu za vijana, awapike anavyotaka.

Hata Maximo ingawa hajalalamika (sababu ya kuogopa kuharibu PR yake) naye anakabiliwa na tatizo hilo, ndo maana kila siku anabadili wachezaji, bila mafanikio.

-------

Kuongezea:

Kwa wachezaji wanaofikiria kuwa kutaniwa ni issue ya kuwavunja moyo, hawana future ya soka. Nilitegemea wangesema watajitahidi kupata hiyo elimu inayotakiwa.

Ifike mahali tuweke na viwango, kuwa kwa mfano kuchezea Yanga lazima mchezaji awe na elimu ya form six at a minimum. Anayesema elimu haichezi mpira, hajui anachoongea. Elimu (si lazima ya darasani - ingawa ya darasani ndio rahisi kuithibithisha (quantify) kwa cheti) ni muhimu kila mahali.

Mchezaji asiye na elimu ya kutosha hawezi kuwa na ambition ya kucheza Ulaya, na kwa ufupi, hatufai, hatusaidii! Nadhani long term stratety ya Yanga iwe ni kuwa-phase out wachezaji wasio-fit kwenye strayety za mwalimu in the next 4 years. Tusisajili tena wachezaji wa mtibwa, simba or any other club, badala yake tusomeshe na kulea vijana wetu wenyewe.

Kwa hilo namuunga mkono kocha 101%. Hakuna sababu ya kuficha matatizo, maana timu itakapo-boronga, atakayelaumiwa ni kocha. Wachezaji kama kawaida yao watadai kocha ni bomu na mafunzo yake hayana mpango, wanamtaka Chamangwana,...,...

Tumesikiliza visingizio vya wachezaji kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita na hatujapa mafanikio yoyote, sasa ifike mahali tukilize na upande wa pili wa wataalamu.

Anonymous said...

Naungana na mtoa maoni hayo ya kwanza hapo juu kwa asilimia mia moja, wala siongezi kitu kwani kasema vizuri mno!!

Anonymous said...

Wachezaji wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha. Kocha ameona kuwa jamaaa lugha haipandi hivyo kuwafundisha inakuwa ngumu sana.

Jambo la msingi sana ni kuwa watu wetu wanapaswa kuwa makini. Hata kama huna elimu bado mtu unaweza kuelewa kama utakuwa makini na kumsikiliza mwalimu. Jamani badilikeni kwa njia ya elimu ndiyo tutafika mbali.

Baba Kelvin, Temboni.