Thursday, February 14, 2008

5 kutokwenda Madagascar

WACHEZAJI watano wa timu ya Yanga wameachwa katika msafara wa timu hiyo unaotarajia kuondoka leo kuelekea Madagascar katika mchezo wa awali Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF) dhidi ya AS Adema.

Wachezaji hao ni Gaudence Mwaikimba, Abuu Ramadhan, Hussein Sued, James Chilapondwa na Laurent Kabanda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lucas Kisasa, alisema wachezaji hao wameachwa kutokana na kuwa majeruhi.

Alisema msafara wao utakuwa na wachezaji 21 na viongozi 8 na utaondoka na ndege ya Shirika ndege la Afrika Kusini, ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega.

Aliwataja wachezaji watakaokuwemo katika msafara huo kuwa ni Benjamin Haule, Jackson Chove, Amir Maftah, Lulanga Mapunda, Abdi Kassim, Vicent Barnabas, Aime Lukunku, Athumani Idd, Jerry Tegete, Waziri Mahadhi, Mrisho Ngassa, Nadir Haroub na Ben Mwalala.

Wengine ni Maurice Sunguti, Hamis Yusuph, Credo Mwaipopo, Abubakar Mtiro, Fred Mbuna, Gula Joshua, Castory Mumbala na Wisdom Ndhlovu.

Aliwataja viongozi watakaoambatana na timu kuwa ni Katibu wa kamati ya Mashindano ya Yanga Emmanuel Mpangala, Katibu Mwenezi Francis Lucas, makocha Dusan Kondic, Spaso Skolovisk, kocha wa watoto,Zivojnov Srdan, Meneja Keneth Mkapa na daktari Sheky Mngazija.

Tunawatakia kila la heri katika michuano hii.

11 comments:

Anonymous said...

Wakati tukiitakia Yanga kila la kheri ktk mchezo wa Jumapili, tunaweza kuongelea hii habari?

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4495

Inahusiana na kusua-sua kwa zoezi la kuingiza wanachama wapya. Inasemekana wanachama hawajitokezi. Lakini mimi nina wasiwasi kama viongozi wametimiza wajibu wao. Je wametembelea wanachama mikoani kuwahamasisha? Au wanadhani wanachama watapeleka tuu hela kwenye matawi ambayo mengine hata hayajulikani makao makuu.?

Nadhani, viongozi wanatakiwa kuweka mkakati maalum, na waonekane wanatekeleza huo makakati. Hata makanisani siku hizi wanafanya jitihada kuongeza sadaka, itakuwa ada ya uanachama ambayo ni hiari.

Binafsi ningependa kuwa mwanachama, lakini niko nje, na sijui kama kuna namna ya kuomba uanachama.

Zack

Anonymous said...

Kuna wachezaji walitoroka kambi Dodoma na kwenda kulewa.Hivi mbona wachezaji wetu hawajifunzi???Tusijali matokeo timua wote wasiokuwa na nidhamu.Bidhamu ndio msingi mkubwa wa maendeleo.Tusijali sura wala jina.

Anonymous said...

NIDHAMU

Anonymous said...

Wapenzi wadau wa blog hii, muda mchache ujao Yanga itajitupa kwenye uwanja wa Mahasima huko Antananarivo Madagascar kupambana na AS Adema ya huko. Panapo majaliwa nitatuma matokeo hapa pindi tu nitakaposikia chochote.

Anonymous said...

Dk 55 mambo bado ni 0-0

Anonymous said...

Dk 67 tupo nyuma bao 1

Anonymous said...

Vipi mpira umeishaje?

Anonymous said...

kama ni 1-0 sii mbaya sana ukizingatia ni ugenini.

Tunaomba matokeo ya mwisho. Simba nao vipi?

Anonymous said...

Kipigo hiki cha 1-0 kisituyumbishe. Tujiandae sasa kupiga mabao hapa nyumbani.

Anonymous said...

Kweli, hakuna sababu ya kushindwa kusonga mbele na kufunga magoli mengi. Maandalizi yawe ya kina timu itakaporudi.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___