Wednesday, February 13, 2008

Safari ya Yanga ni kesho

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Madagascar kwenye mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Adema utakaochezwa Jumapili kwa ndege ya Shirika la ndege la Afrika Kusini.

Kikosi hicho kitaondoka nchini kwa ndege ya Shirika la ndege la Afrika ya Kusini SAA.

Awali, uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kuwa timu hiyo ingeondoka nchini kwa kutumia ndege ya serikali siku moja kabla ya mchezo wao huo, ambapo ingerejea mara baada ya mchezo wake kumalizika.

Hata hivyo wakala wa ndege za serikali walitoa taarifa kwa uongozi wa klabu hiyo kuwa haitawezekana kupata ndege ya serikali kwa siku hiyo, ambapo uongozi ulitakiwa kutafuta ndege nyingine.

Yanga inatarajia kuondoka na msafara watu 30, kati ya hao 21 ni wachezaji.

4 comments:

Anonymous said...

Kila la kheri.

Tunaweza kupata live coverage kupitia hapa?

Anonymous said...

je utaona hii mechi ya yanga simba tulio hapa marekani mimi nitanunua kupitia internet ,because its going to be death match for simba,tafadhali mnijulishe asante .mwanza

CM said...

Anon wa kwanza - kama muda utapatikana nitajitahidi kutuma matokeo kama ninavyofanya wakati wa mechi za ligi kuu ya Vodacom.

Anon wa pili - mechi hiyo ya Yanga na Simba itapigwa Aprili 27.

Akhsante.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___