Wednesday, February 06, 2008

Hii nayo vipi?
Baada ya wachezaji wawili wa klabu ya soka ya Yanga Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa kusimamishwa kuichezea klabu hiyo, kwa kipindi cha miezi sita kwa madai ya utovu wa nidhamu, uongozi wa klabu hiyo una mpango wa kuwatimua wengine watatu zaidi.

Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Rashindi Ngozoma Matunda alisema kuwa wachezaji hao wanatuhumiwa kwa siku nyingi kuuza mechi za dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Matunda, ambaye aliwataja wachezaji hao (majina tunayahifadhi) kwa kueleza kuwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana na viongozi wawili wa zamani kuuza mechi ili waendelee kufungwa na watani wao.

Alisema kuwa wachezaji hao ndio waliokuwa wanatumika kama 'rimoti' katika kuifungisha Yanga huku wakiwa wamechukua mamilioni ya fedha kutoka wapinzani wao.

Matunda alisema kuwa wachezaji hao mara zote walikuwa wanajua kabla kwamba mechi wanayokwenda kucheza watafungwa au kutoka sare kutokana na maelekezo ambayo walikuwa wanapewa na viongozi hao wa zamani.

Alisema kuwa wachezaji hao wapo katika orodha ya kufukuzwa katika klabu hiyo kutokana na kutuhumiwa kuhusika kuhujumu Yanga kwa muda mrefu sana.

``Sisi baada ya kuingia madarakani tulifanya uchunguzi kwa nini tunafungwa na Simba kila mara, baadae tulipata orodha ya wachezaji watano ambayo ndio waliokuwa wanafungisha timu yetu,`` alisema Matunda.

Yanga kwa kipindi cha miaka saba hawajaweza kuwafunga watani wao wa jadi Simba katika mchezo wa Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara.
  • SOURCE: Nipashe

3 comments:

Anonymous said...

watajwe hao wasaliti.

Anonymous said...

Huyu Matunda asifanye watu wajinga.Tangu wameingia madarakani tumefungwa na Simba mara mbili alikuwa wapi kusema hayo??Asifikiri wanayanga bado wanaamini tambo zake za hirizi na nguvu za giza.Tumefungwa kimpira .Mpira ni sayansi sio matunguli.Tujitayarishe vizuri tujenge timu kisayansi.Hao waganga njaa watakimbia wenyewe.Tafuteni kazi wacheni kuifanya Yanga mradi wa kutafutia maisha.

Anonymous said...

Mdau wa pili hapo juu, nakubaliana nawe 110%.

Huyu Mzee amechoka, badala ya kuleta sababu za kisayansi yeye anakimbilia upuuzi.! Hawa ndo wanawatia wachezaji hofu wakati wa mechi za Simba hadi wanashindwa kucheza mpira sawasawa.