Friday, February 08, 2008

Yanga na Polisi DOM leo

YANGA, leo itakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kumenyana na Polisi ya huko katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mjini Dodoma, Yanga itakuwa na kazi moja ya kusaka ushindi ili kuzidi kuipumulia Prisons inayoongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 30. Yanga ipo nafasi ya pili, ikiwa na pointi 27, ikishinda mechi hiyo italingana pointi na Prisons. Hata hivyo, Prisons ina mabao mengi ya kufunga kwani imepachika mabao 23 na Yanga imefunga 16.

Kimtazamo, mechi hiyo inaonekana kuwa rahisi kwa wakali hao wa Jangwani hasa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Septemba 30 mwaka jana kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Polisi Dodoma hivi sasa inanolewa na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Yanga Sekilojo Chambua. Tunachojiuliza ni je, atatuwekea ngumu?


9 comments:

Anonymous said...

mechi inaendeleaje?
-mosonga

Anonymous said...

Tumeshinda 3-0

Anonymous said...

Opps, thanx kwa hizi habari. Nilikuwa bize na mambo ya bungeni nikasahau chama langu. Naona mbio nzuri, sidhani kama prisons wataweza hii speed yetu. Vipi wafungaji kina nani?

Anonymous said...

jamani tuleteeni analysis

Anonymous said...

Wafungaji ni beki Mmalawi Wisdom Ndlovu, Fred Mbuna na Castory Mumbala.

Anonymous said...

Prisona nae kamtungua Manyema goli4-1.Mambo bado kabisa.

Anonymous said...

Ndugu wapenzi hasa wahusika wa kupost taarifa katika blog hii nawaomba muwe up to date. Maana blog yetu inakosa taarifa current na imekosa picha muhimu za club yetu kama picha za wachezaji, kikosi kizima, picha za makocha na viongozi nk.

Anonymous said...

Ku-update habari kila mara (latest) -inategemea kama wahusika wako TZ au nje ya nchi au upatikanaji nafasi.
Hata hivyo wanajitahidi saana kutuletea habari za klabu yetu.
Hongereni jamani, hiki tunachokisoma hapa si haba!!

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___