Tuesday, February 19, 2008

Kifo cha Simba Machi 30

Mechi marudiano ya Ligi Kuu ya Vodacom baina ya Simba na Yanga itachezwa Machi 30 badala ya Aprili kutokana na utashi wa kituo cha televisheni ya malipo cha GTV, ambacho kitaionyesha mechi hiyo moja kwa moja .

Awali, mchezo huo baina ya vigogo hivyo vya soka soka nchini, ilikuwa imepangwa kufanyika Aprili 27, lakini afisa habari wa Shirikisho la Soka (TFF), Florian Kaijage alisema ombi la GTV la kutaka mchezo ufanyike Jumapili ili uweze kuonyeshwa moja kwa moja na kituo hicho cha televisheni, limekubaliwa.

Katika hatua nyingine, uongozi wa klabu ya Yanga umeandika barua TFF kuomba kusongezwa mbele kwa mechi zake tatu, lakini shirikisho hilo limekubali kusogeza mbele mechi yao na Kagera Sugar, iliyopangwa kufanyika keshokutwa mjini Bukoba.

Alisema mechi nyingine dhidi ya Toto Africans itachezwa Februari 23 badala ya 24 kama ilivyotangazwa mwanzo na dhidi ya Mtibwa itakuwa Februari 27 badala ya 28.

Alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa Yanga muda wa siku tatu wa kujiandaa na mashindano ya kimataifa na kwa mujibu wa kanuni za (TFF) Yanga wanatakiwa kupumzika siku tatu kabla mchezo wa marudiano.

3 comments:

Anonymous said...

Kwa mpira huu tunaocheza na ubabaishaji wa viongozi tuna kazi kubwa.Huko Dodoma Ken Mkapa meneja wa timu aliruhusu wachezaji watoroke kwenda Disco halafu bado tunajitapa.Kocha kalalamika hakuna hatua zinachukuliwa.Tukifungwa kama kawaida tutatafuta mchawi.Mechi ya Simba kwa vingozi na wazee waganga njaa ni biashara.Hivyo lolote linaweza kutokea.Tuache majigambo.Tutayarishe timu kisayansi.Bila hvyo kuna kila dalili ya kuudhika tena.

Anonymous said...

Kisoka tuko juu zaidi ya Simba hii inamaanisha kuwa hiyo tarehe 30 itakuwa mwisho wa uteja.

Anonymous said...

Miaka saba tulidai hivyo na tunaishia kulizwa.Maadui wa Yanga wapo ndani ya Yanga wachezaji na viongozi fulani.Bila kuwasafisha ushindi ni ndoto.