Saturday, February 02, 2008

Tumeshindilia 4-0Jerry Tegete "Kayumba"
ana mabao 3 ktk mechi 2.

Vijana wa Jangwani Yanga jana waliishindilia Coastal Union ya Tanga kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Maurice Sunguti, Abuu Ramadhani na Jerry Tegete 'Kayumba'.

Kwa ushindi huo sasa Yanga imefikisha pointi 27 sawa na Prisons ya Mbeya inayoongoza ligi hiyo kwa tofauti ya magoli.

Kazi nzuri sana vijana, tupeni raha.

13 comments:

Anonymous said...

Waungwana, wenzetu mliokuwa uwanjani hebu tupeni habari timu ilichezaje? Ingawaje pamoja na kuwa mbali nafikiri walimu ni wazuri maana nikitazama timu iliyocheza napata picha kuwa hawa jamaa wanapanga mtu kutokana na wanavyomuona juhudi zake mazoezini, maana ingekuwa Chamangwana hapa tungeona majina ya akina Mwaikimba, Mwalala wakati wala hatuoni kitu. Tuwape nafasi waibadilishe timu

Anonymous said...

1. Nilisema wakati watu wanaponda kiwango baada ya mechi ya Ashanti last week kwamba tuipe timu mechi 3 tuone kama kweli hawajafanya kazi au vipi! Mechi ya pili nadhani inaonesha mwelekeo mzuri. Waliokuwa uwanjani tunaomba analysis ya uchezaji/kiwango cha timu.

2. Huyu Jerry ni mchezaji mzuri kweli. Bado ni mdogo na nadhani anapokea mafunzo kirahisi kuliko kina Mwalala na Sunguti. Alionwa na Micho enzi zile, akasema asainishwe mkataba ingawa hakukuwa na nafasi (kumbuka wakati ule alishasaini Simba). Viongozi kama kawaida walikuwa wanakimbilia majina makubwa na kuacha chipukizi wenye potential.

3. Tuwaenzi makocha wanaotoa nafasi kwa mchezaji kulingana na uwezo wake badala ya umaarufu wa jina.

Anonymous said...

Hiki cha kutopanga kwa majina kimenifurahisha saana, nafikiri itawapa moyo na watu wafanye mazoezi kwa nguvu

Anonymous said...

Mpaka hapo shwari chama yetu!

Anonymous said...

nafatilizia kwa mbali naona maendeleo yanakuja nashauri kuwa na subira kibaden kakiri kuwa yanga ni timu pekee inayocheza mpira wa kisasa nawatakia kila la kheri ni mwaka wa simba kula 5 kama 1968 inshaallah

Anonymous said...

Tuache mpira wa mdomo.Nilikuwepo kiwanjani na sijaona bado mabadiliko ya kuridhisha au kusifia.Tumecheza na timu mbili ambazo hazina kiwango cha juu sana kwa jinsi nilivyoona zinacheza.Jerry ni mchezaji mzuri sana lakini alicheleweshwa kuingia.Timu bado sana hasa viungo na walinzi na kipa.Wakicheza na timu kali tutapata matatizo.Tujenge timu taratibu lakini stori za Ali nacha hazijengi.

Anonymous said...

Mdau hapo juu, maoni yako yana mantiki. Kwamba tusikalie kusifu tuu tukasahau kurekebisha makosa. Lakini si timu hizi zilizotufunga round iliyopita? Sasa tunapoifunga timu hiyo magoli 4-0, halafu ukasema hujaona mabadiliko yoyote (ya kuridhisha/kusifia), hapo sielewi.

Mabadiliko ya kweli huenda tutayaona baada ya muda kidogo, lakini hata yale madogo, basi tuwape moyo makocha na wachezaji, ili wajitahidi zaidi.

Anonymous said...

Niliona mechi ya Tanga pia.COASTAL WALICHEZA VIZURI SANA TOFAUTI NA MECHI WALIYOCHEZA DAR.Udhaifu mkubwa wa Coastal kwa sasa ndio umetufanya tuonekane kwamba timu ni nzuri.Uliona mechi ya Dar???Tutakapocheza na timu ngumu ndio tutaona udhaifu wetu lakini kwa sasa ni mapema sana kusifia.Kwani wachezaji wetu wana udhaifu wakianza kusifiwa kama mnavyofanya sasa wataanza kulewa sifa.Mimi bado sijaona cha kusifia.Tucheza na timu ngumu tucheze vizuri.Tatizo la viungo bado sana.Chuji na Tegete ndio wachezaji ambao wanafaa kuchezea Yanga ninayoitarajia.Wengine bado sana.

Anonymous said...

Shukurani kwa kutufungua macho, sasa na huyu Yusuf Hamisi un asemaje? Nafikiri tatizo kubwa la timu zetu ni pale wachezaji wanasajiliwa kwa matakwa ya viongozi na si kocha. Kocha husajili wachezaji ambao wataendana na mfumo wa uchezaji anaoutaka. Nafikiri sasa mtakubali manmeno ya Kodic ingawaje yanauma.

Anonymous said...

Hii habari ya Manji kujifanya kocha inatia wasiwasi.Inasemekana ameongea na baadhi ya wachezaji na kuwatishia kwamba viwango vyao haviridhishi hivyo wanaweza kukuta wanatimuliwa.Je hiyo sio kazi ya kocha???Kwenye timu za wenzetu mfadhili anafadhili timu full stop.Masuala ya uchezaji na wachezaji kuna kocha na jopo lake.Tuanze kuziba ufa kabla ya kujenga ukuta.

Anonymous said...

Kwanza sijafurahishwa na kumwita Tegete "Kayumba". Sijui umelitoa wapi ili jina.

Yanga kwa wastani hawajacheza vizuri sana lakini kama timu wanaenda vizuri.
1. Kwanza timu imeanza kucheza kama timu sio mtu mmoja mmoja. Hii inafaida sana maana hata kama mchezaji mmoja hakitoka bado timu haiyumbi.

2. Yanga sasa wana some creativity katika uchezaji wao. Unaona wanatengeneza nafasi fulani fulani.

3. Tatizo linalowakabili bado ni wepesi na umakini. Yusuf Hamis, Credo na Aboou siku ile walilaumiwa sana na mashabiki. Ni kweli walikuwa wanapoteza pasi nyingi. Lakini ni katika kujifunza. Kwangu Yusuf na Credo walitimiza wajibu wao wa msingi vizuri kabisa, ambao ni kunyang'anya mipira. Ule wa pili ndio ulikuwa na matatizo ambao ni kutoa pasi. Naamini mwalimu ataweka concentration kwenye ilo na siku zijazo wanaweza kucheza vizuri zaidi.

Kwa wastani Yanga ni nzuri kwa sasa kuliko ilivyokuwa.

Anonymous said...

Jina la Kayumba amepewa na wachezaji wenzake kwa vile bado ni wakusoma. Tegete akitoka shule ndiyo anakwenda mazoezini.

Anonymous said...

Kwa faida yake bora usilivumishe ili life