Thursday, March 13, 2008

Baba na mwana leo

Yanga leo inajitupa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kupambana na watoto wao Pan Africans katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Yanga yenye pointi 40 hadi sasa inatarajia kuendeleza wimbi lake wa ushindi kwani tangu raundi ya pili imeanza imepoteza pointi 2 tu.

Tunatarajia mzee wetu Sunguti leo ataendeleza rekodi yake ya ufungaji. Hivi sasa anashikilia nafasi ya pili akiwa nyuma ya Yona Ndabila wa Prisons kwa tofauti ya goli moja. Ndabila amefunga mabao 8.

Pan Africa haipo katika nafasi nzuri katika ligi hiyo hivyo nayo si timu ya kubeza. Tunatarajia mchezo mzuri na panapo majaliwa mwisho wa siku tuondoke na pointi zetu 3.

20 comments:

Anonymous said...

mambo vipi huko?

Anonymous said...

Vipi matokeo mpaka sasa kuko u/taifa?

Anonymous said...

nadhani bado mpira unandelea, kipindi cha pili, vipi maendeleo (magoli).

Anonymous said...

Mheshimiwa CM labda hana mtandao uko uwanjani, wacha tusubiri...

CM said...

Tunaongoza 2-1. Hivi sasa ni dk ya 69.

Samahani kwa ukimya ndugu zangu

Anonymous said...

Hey, thanks ....

Anonymous said...

Hey, thanks ....

CM said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-1.

Mabao mawili yaliyofungwa na Mrisho Ngassa leo yametubeba baada ya Pan Africa kutangulia kufunga.

Kwa ushindi huu sasa tumefikisha pointi 43. Tukiwa tumewaacha Prisons kwa tofauti ya pointi 5.

Anonymous said...

vita mbele nyuma mwiko vijana wameahidi na matokeo yanaonekana kila la kheri wana yanga wote
m.sakran kuwait

Anonymous said...

Good keep it up

Anonymous said...

Asante kwa matokeo mzee.
Mdau, UK

Anonymous said...

Shukrani kwa taarifa, na pongezi nyingi kwa wachezaji kwa kutupa raha. Mwendo huo huo hadi mwisho.

Anonymous said...

Jamani, pamoja kuwa tunafurahia huu ushindi mimi napenda kuuliza waliokuwa uwanjani na ambao wamekuwa wakiona mechi za Yanga, hivi tatizo ni nini? mbona tunaruhusu mabao kufungwa hata na timu mbovu?
Hawa Pan si walipingwa nne na watani wetu Simba?
naelewa tatizo la timu kusajiliwa na viongozo, let hope Kondic asajili anaowataka ili tuone

Anonymous said...

Nilikuwepo uwanjani, mechi ilikuwa ngumu sana. Huwezi kuamini, Pan walipania kupita kiasi. Hata hivyo, nampongeza sana Kondik kwani mfumo wa 4-3-3 jana ulionyesha kukubali sana hasa kwenye kiungo. Abdi Kassim na Mumbala waling'ara sana na pia pale mbele kulia Ngassa alicheza vizuri sana. Kwa maoni yangu, Abdi Kassim alikuwa nyota wa mchezo. Nadhani kikosi cha jana kikiimarishwa na Chuji na Barbabas ambao jana hawakucheza, ndicho cha ushindi.

Anonymous said...

Kufungwa goli na Pan si hoja. Cha msingi tumeshinda. Kuna mifano mingi timu za chini kuzigomea timu kubwa:
Wigan 0 Arsenal 0,
Derby 1 L/pool 2,
Birmingham 2 Arsenal 2,
Getafe (Spain) ilimfunga Real Madrid n.k.
Cha msingi ni Yanga kucheza vizuri na ktumia vema nafasi wanazozipata.
Kwa sasa kila timu nchini ingependa iifunge Yanga ili kujitengenezea jina!
Mi naona mambo yako safi Yanga, na nafasi ya ubingwa ni kubwa sana!

Anonymous said...

Kitendo cha baadhi ya wanachama kuwatishia wachezaji maisha ni kitendo cha kulaaniwa kwani kinafanya wachezaji wetu wawe na mchecheto wakicheza na Simba.Kuwatishia Mtiro, Credo, Mbuna na Mahadhi sio tu kinawaathiri wachezaji wengine kisaikolojia bali kinakatisha tamaa wachezaji wengine kucheza vizuri kwani kunakuwa na hofu kwamba ukikosea utapachikwa usaliti.

Anonymous said...

mbaya sana kuwatisha washezaji mpira ndivyo ulivyo siku game inakubali siku inakataa ndo hivyo yani tuondoe dhana ya kuwatisha hawa naamini wanamoyo na nia ya kuifikisha yanga mbali cha msingi walinde viwango

Anonymous said...

ndugu yetu mwanayanga tafadhali utupe hali halisi ya uchezaji wa yanga maana ukisoma magazeti mengine wanasema yanga mbovu,sasa hii inatuvunja moyo nainatutisha wakati tukicheza na yule myama. asante. mwanza

Anonymous said...

Mimi kwa muono wangu nadhani Tegete anasitahili kucheza zaidi. Ni mzuri kujipanga na kuscore kuliko forward wengi pale yanga. Halafu kocha anatakiwa kuwafundisha wachezaji kucheza kwwa kufuata vipaji vya wachezaji walipitiliza kama ngassa. Naona wachezaji wengi hawatumii speed ya ngassa kujipanga na kufunga. Akienda kasi wao wanakuwa kama wanamshangaa na anapoingiza mipira inawakuta off balance. Kidogo tegete amekuwa akifuata sana kasi ya ngassa na magori yake mengi kapata mapande ya Ngassa. Kocha naona ni mzito wa kufanya maamuzi. Nimeona mechi ya adema, abuu alikufa mapema lakini akachelewa kufanya maamuzi yaliyosababisha baazi ya wachezaji kucheza kwa nguvu na kuumia ovyo wakati wa kusaka ushindi.

Anonymous said...

Maoni mazuri wadau, keep it up.