Thursday, March 13, 2008

Safari ni Machi 18

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini Machi 18 kwenda nchini Libya kwenye mchezo wake wa kwanza wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Akhdar ya nchini humo katika mchezo utakaochezwa Machi 21 kwenye uwanja wa Al Bayda uliopo katika jiji la Tripoli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Lucas Kisasa alisema kuwa uongozi unashughulikia suala la ndege , ambayo itawapeleka nchini humo.

Kisasa, alisema kuwa wanatarajia kuondoka na wachezaji wote watakaoteuliwa na kocha, ambapo baadhi ya wachezaji ambao ni majeruhi wataachwa ili kuendelea kupatiwa matibabu.

Alisema wameamua kwenda huko siku tatu kabla ya mchezo ili kukabiliana na mazingira ya huko, ikiwa ni pamoja na kuzoea hali ya hewa.

No comments: