Tuesday, March 11, 2008

CAF 'yasogeza mbele kifo cha Simba

Pambano la watani wa jadi la Yanga na Simba limeingia matatani kufanyika Machi 30 mwaka huu baada ya Shirikisho la soka la Afrika CAF kufanya mabadiliko ya ghafla katika ratiba ya michuano ya kufuzu kwa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa mechi hiyo itafanyika kati ya Machi 28 na Machi 30 mwaka huu, ambapo mchezo wa kwanza utafanyika Nairobi Kenya na kurudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili baadaye.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage iwapo Taifa Stars itaitoa Kenya itakwaana na mshindi kati ya Uganda na Eritrea.

Mchezo huo utafanyika nchini Kati ya Mei 2 na Mei 4 mwaka huu hapa nchini na kurudiwa wiki mbili baadaye nchini Eritrea.

Hapo awali TFF ilipanga pambano la watani wa jadi (Yanga na Simba) kufanyika Aprili 27 lakini wadhamini wenza wa ligi hiyo GTV waliomba pambano hilo lipigwe Machi 30.

Tusubiri tuone tarehe mpya.

4 comments:

Anonymous said...

tunaomba blog hii iwekwaajili ya kutufahamisha wapenziwa yanga mbambo yote yanayoendelea michezoni pamoja na matokeo ya michezo yote pamoja na kuweka msimamo wa ligi na ratiba za michezo ili kutuwezesha wapezi wa yanga popote duniani kujua habari zinavyoendeleaza michezo kwani nadhani hakuta web mahususi kwa ajili ya michezo Tanzania

Anonymous said...

Ni miaka 7 tangu mnyama aanze kutunyanyasa.Wakati wa kampeni za walio madarakani kwa hivi sasa, baadhi ya WAZEE maarufu waliahidi tukiwachagua Mnyama hatafurukuta kwani wao ni muarobaini!!!! Last time walipewa 10m.kuandaa mazingira ya ushindi,Mwakingwe akawabeza!!! Safari hii je? tusidanganyane, viongozi na wazee kuweni wa kweli, mmeshindwa kupata muarobaini, ombeni msaada kwa wanachama wakeleketwa. MZIMBA, MATUNDA,.....MPOOOO!!!!

Wachezaji wameanza kuonekana na Friends of Simba kuna matumaini hapo???Suala hili lipatiwe ufumbuzi wa kina ama sivyo tutalizwa tena.Walikuwa wanafanya nini kwenye magari ya mahasidi wetu??Tusipoziba ufa tutajenga ukuta.