Kibaruani Moro leo
Yanga leo inajitupa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kucheza na Moro United katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga yenye pointi 37 itataka kushinda mchezo huo ili kujiweka kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo, huku Moro United nayo itataka ishinde ili iwe moja ya timu zilizo kwenye nafasi za juu.
Mchezo wa Morogoro unatarajiwa kuwa na upinzani mkali zaidi, ambapo bila shaka mashabiki watakaohudhuria watapata burudani ya nguvu.
Ni wazi kuwa washambuliaji wa Moro United wakiongozwa na Nsa Job na Herry Morris watakuwa na uchu wa mabao, huku wale wa Yanga wakiongozwa na Maurice Sunguti, Abdi Kassim na Abuu Ramadhani nao watataka kuendelea kuipaisha Yanga.
Yote juu ya yote tunawatakia ushindi vijana wetu.
8 comments:
Wajomba tunasubiri toka Morogoro tusikie
aany result please?
tunaongoza kwa mabao mawili huko Moro
Bado tunaongoza 2-1 hivi sasa ni dakika ya 77
Mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-1.
tuna wapa pongezi wachezaji wetu kwa ushindi kila la kheri Yanga
Mechi yetu na Simba huenda likasogezwa mbele kwa ajili ya kupisha mechi kati ya Taifa Stars na Harambee Stars. Mengi zaidi kesho.
Huu nuitakuwa utoto mkubwa saana, timu ya taifa haika kalenda? yaani iknakuwa kama mtu kashikwa na tumbo la kuharisha kuwa hujui ni wakati gani utahitajika kwenda msalaani?
Post a Comment