Saturday, March 22, 2008

Pasaka njema
Hamis Yusuf
Mfungaji wa bao la kusawazisha

Tunawashukuru sana wachezaji wa Yanga kwa kutuingiza katika sikukuu ya Pasaka kwa furaha.

Hata hivyo licha ya kutoka sare ya 1- 1 katika mchezo wa jana dhidi ya Al Akhdar ya Libya bado Yanga inahitaji kufanya kazi katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo.

Endapo Yanga itarejea nchini na kumwagiwa sifa kwa sare yao ya 1-1 basi hii itawarahisishia kazi Al Akhdar ambao watakuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya 'kujikomboa' na balaa la kung'oka katika michuano hii.

Dawa ni kukaza buti, mapambano yanaendelea.

PASAKA NJEMA KWA WADAU WOTE POPOTE PALE MLIPO.


3 comments:

John kapota said...

Tusibweteke! sisi tumeweza kutoka nao sare kwao nao vilevile wanaweza kuja kufanya lolote kwetu mpira unadunda. Muhimu kufanya maandalizi mazuri kwa mechi ya marudiano.

Anonymous said...

fanyeni kweli hamuoni pesa zina mwagwa na mfadhili wenu? halafu mubolonge katika mechi zenu si ndio mwanzo wa kumfukuza huyo mfadhili? mtapata wapi posho,mishahara,kambi nzuri, basi fanyeni kweli ili muweze kula vilivyo nona kwa mfadhil hiyo.Endapo mtafanya vizuri katika mechi zilizo bakia hapo ndipo mtamfurahisha mfadhili huyo na kuendelea kula vilivyo nona.WACHEZAJI JITUMENI UWANJANI KAMA MNAVYOJITUMA KUCHUKUA MISHARA YENU.MNAPENDA KUSAFIRI NA NDEGE? BASI FANYENI KWELI ILI MUENDELEE KUSAFILI NAMUTANGAZE VIPAJI VYENU. MKIFIKILIA HILO TU BASI MTAFAFIKA MBALI.
BAY RAYMOND kweka kutoka kitakuru.

Anonymous said...

natabiri wakati huu ni goli 5 .