Tuesday, March 18, 2008

Safarini Libya
Wakati timu ya Yanga ikiondoka leo mchana kuelekea Libya katika mchezo wake wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), dhidi ya Al- Akhdar, hadi jana jioni bado Kocha Mkuu wa timu hiyo Dusan Kondic alikuwa hajapata kikosi kamili kutokana na majeruhi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lucas Kisasa alisema mipango yote ya safari imekamilika na timu itaondoka na wachezaji 18, lakini hadi jana bado Kondic alikuwa hajatangaza kikosi kutokana na kuwa na majeruhi wengi.

Kisasa alisema hawezi kutangaza majina ya wachezaji kwa kuwa bado hajakabidhiwa na kocha kutokana na kuwa na majeruhi wengi, kitu ambacho alikuwa anafanya tathmini ya wachezaji watakaoziba mapengo ya majeruhi hao. Miongoni mwa wachezaji ambao ni majeruhi ni kiungo mahiri Athumani Idd 'Chuji'.

Alisema msafara utakuwa na watu 26 na utaondoka leo alasiri, ambapo kwa upande wa viongozi kutakuwa na Katibu wa kamati ya Mashindano ya Yanga, Emmanuel Mpangala na Katibu Mkuu Lucas Kisasa, wakati Mkuu wa Msafara atakuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Theofred Sikazwe.

Sikazwe alikataliwa na uongozi wa klabu ya Simba wakati ikienda Ethiopia kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Awasa City, kwa kile uongozi huo ilichodai wana taratibu zao.

18 comments:

Anonymous said...

Kila la heri Yanga. Sijui kama tulioko nje ya TZ tunaweza kufuatilia matangazo ya mchezo?
Kama haiwezekani CM tusaidie kama kawaida tafadhali.

Anonymous said...

tunawatakia kila la kheri iwe safari ya mafanikio mtatujulisha matokeo kama kawaida m sakran kuwait

Anonymous said...

Hivi Mwalala ana matatizo gani? mbona simsikii kapangwa? ukweli nimefurahia saana upangaji wa Kondic hamna kupanga kwa majina, nafikiri kama Mwalala haumwi au la basi ni mwafaka Yanga kumwacha kwenye usajili

Anonymous said...

Kwa wenye ma dish makubwa mechi hii inaweza kuonyeshwa ta TV za kiarabu, huwa zinaonyesha sana mechi za North Africa.

Kuhusu Mwalala, amekuwa ni mzigo mkubwa. Mara ya mwisho alipopangwa siku ya mechi ya Mtibwa alikuwa mzito mno. Akinyang'anywa mpira hakabi, badala yake anainama na kujishika magoti kama mtu aliyeumia, na ndivyo alivyo siku zote! Pili, amenenepa sana. Na pia alionyesha utovu mkubwa wa nidhamu kwani alipotolewa na kocha, aligoma kwenda kukaa bench na akakataa hata maji huku akipunga mkono kwa hasira. Ametimiza vigezo vyote vya kuachwa next season kwa utovu wake wa nidhamu. Katika foreigners tulionao, Sunguti na Ndlovu wanajituma sana.

Anonymous said...

that was very good comments.asante

Anonymous said...

wishing you all the best

Anonymous said...

dakika 29 kipindi cha kwanza bado bila bila na vijana wanashambulia inshaallah ushindi upo

Anonymous said...

Dakika zilizokwenda hadi sasa ni 31 bado ni 0-0.

Game linatangazwa na radio ya TBC (RTD)

Anonymous said...

HT 0-0

Anonymous said...

game half time 0-0tv libya watangazaji wana khofu kipindi cha pili maana yanga wamekosa magoli matatu ambayo kipa amejitahidi kuokoa hatari za yanga kila la kheri kwa wana jangwani

Anonymous said...

dakika ya pili akhdar wamepata goli 1

Anonymous said...

1+1 dakika ya 18 kipindi cha pili

Anonymous said...

mpira umekwisha ngoma drew 1+1 mpira wa marudiano mpira ulikuwa mzuri nawatakia kila la kheri katika marudiano dar m sakran kuwait

Anonymous said...

Tunakushukuru sana mdau wa Kuwait, tumekupata vizuri.

Yanga Imara Daima.

CM

Anonymous said...

Du asante sana kwa matokeo na hongera
sana vijana wa jangani marudiano ni kichapo tu kila la heri mdau cuba

Anonymous said...

NANI ALIKUA MFUNGAJI?

Anonymous said...

Aise saafi sana...

Shukrani sakram, huu ndo umuhimu wa blog au mnasemaje wadau? Vipi timu imechezaje? Nani kafunga bao letu.. etc?

Haya ni matokeo mazuri, maana hata sare ya bila mabao mchezo ujao inatuvusha. Ila ushauri wangu ni: Wachezaji wasibweteke na hii droo, maana jamaa wakija Dar wakatangulia kutufunga bao, itafanya mchezo uwe mgumu. Timu iandaliwe kushinda mechi ijayo tena kwa mabao mengi...

Yanga Daima Mbele..


Zack, USA.

Anonymous said...

Dah! shwari kama matokeo ndio hayo, hapa kinachotakiwa ni kugangamala kuwapa goli 3 mtungi ili tusonge, hapa ndio unakuja umuhimu wa blog asante sana mdau muanzilishi wa blog hii.
Kila la heri wana Yanga wote, mungu yupo nasi ktk ushindi mechi ya marudiano, asante pia mdau wa Kuwait kwa taarifa za matokeo.
Mwana Yanga halisi,
Japan.