Thursday, April 10, 2008

Bado pointi 4 tu


KAMATI ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetengua uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo kuirejesheshea timu ya Simba ushindi wa mabao pointi tatu na mabao mawili kutokana na mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kutokana na uamuzi huo Coastal Union inafikisha pointi 25 ingawa bado inashika nafasi ya pili kutoka chini, huku Simba yenye pointi 37 ikishuka hadi pointi 34 ikiwa na michezo minne mkononi.

Kama Simba ikishinda michezo yake minne iliyoshinda itafikisha pointi 46 na hivyo kujiweka katika wakati mgumu wa kutwaa ubingwa, kwani Yanga yenye pointi 43 na michezo mitano mkononi, inahitaji pointi nne tu kutwaa ubingwa.

Wakati huo huo, lile pambano kati ya Yanga na Manyema lililovunjika hapo jana kutokana na maji yaliyotokana na mvua kunyesha sasa litapigwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa Jijini.

9 comments:

Anonymous said...

Hongera Yanga; hilo kombe ni letu, hakuna wasi!!! Ila timu itafute 'dawa' ili klabu bingwa mwakani tufike mbali.

Kwa mawazo yangu, 'dawa' ni kujitengenezea vitega uchumi vya maana ili timu ijiingizie fedha. Yanga ikiweza kujiwekea vitega uchumi, itaweza kujipatia maendeleo makubwa. Kwa mfano:
-tutawavutia wachezaji wengi bora kuja Yanga
-tutasajili wachezaji wazuri
-tutawalipa vizuri wachezaji
-watapata moyo na ari ya kujituma zaidi
-timu itajijengea kituo kizuri cha mazoezi ya kisasa kwa wachezaji
-timu itapunguza utegemezi wa wafadhili.
-n.k.

Timu haiwezi kuendelea kwa kutegemea utashi wa wafadhili kila wakati. Ni lazima Yanga iwe na chanzo chake cha mapato cha uhakika.

Sina ugomvi Yanga kupata misaada kutoka kwa wahisani, na (nadhani) hata wahisani hawana tatizo kama timu itajitafutia vyanzo vya kudumu vya fedha!

Anonymous said...

Mdau hapo juu nakubaliana nawe asilimia 101.

Anonymous said...

Huo mpira leo upo na ni mvua kama jana?

Anonymous said...

hakuna mvua na kwa bahati mbaya mpira hautangazwi redioni hivyo basi tutachelewa kidogo kuwapatia matokeo.

Anonymous said...

Nakubaliana na mawazo ya hapo juu pia nasubiri matokeo maana nina dukuduku furaha zaidi kumuua mnyama ili wajue kunyamaza kila wanapopoteza mechi maneno yao ni yanga m sakran kuwait

Anonymous said...

Vp mbona kimya jamani. Vp matokeo?

Anonymous said...

Tumeshinda 1-0, bao lililofungwa na Abdi Kassim 'Babbi' ktk dk ya 9.

Kwa ushindi huu, sasa tunahitaji pt.1 katika mechi 4.

CM

Anonymous said...

Aksante kwa matokeo na pongezi kwa wachezaji wetu.

Sasa kwa vile tunahitaji point 1 ambayo najua itapatikana mechi ijayo, nadhani muda muafaka wa kuanza kujipanga kwa ajili ya ligi ya mabingwa mwakani.

Mdau wa kwanza pale juu ametoa maoni ya muhimu sana. I wish viongozi wangekuwa wanapita humu na kuchukua mawili-matatu. nami naongezea yafuatayo:

1. Napendekeza timu ianze kuandaliwa kwa ajili ya ligi ya mabigwa mara tuu baada ya ligi kuu. Napendekeza usajiri wa wachezaji wapya ulenge zaidi vijana ambao watachezea Yanga kwa miaka hadi 6 ijayo. Kwa hiyo ningetegemea wachezaji wapya watakaosajiliwa ni watoke kwenye list ya wachezaji wa Chamangwana (wale waliotokana na kombe la Copa Coca Cola mwaka jana).

Hao wajaze nafasi za kina Mwaikimba na Mwalala. Wawekwe kambini ndani na nje ya nchi tangu July nadi ligi kuu itakapoanza tena. Naamini baada ya hapo tutaweza angalau kuingia kwenye ligi ya mabingwa, na kwa kuwa wachezaji hawa watakuwa bado wadogo kwa umri, itakuwa rahisi kwao kujifunza na kuongeza ujuzi kila mwaka.

2. Nashauri pia wasajiriwe wachezaji 25 tuu ( maana ndio hao tunaohitaji kucheza ligi ya ndani na mashindano ya Afrika), ila wawepo na reserve (vijana) wengine 10 wakitafuta namba, hawa wawe wanatrain pamoja na timu na wapewe namba kulingana na hali itakavyokuwa wakati wa mashindano, kama kuziba nafasi ya walioumia n.k. Windows za kuongeza wachezaji zipo nyingi.

Kutakuwa na argument kwamba tunahitaji wachezaji wazoefu. Ni kweli, lakini kama hatuwezi kuwapata toka nchi zilizotuzidi kisoka(kama Congo, Ghana, Cameroom, Ivory Coast, etc), hawa wa Kenya na Uganda wanagharama tuu, bila msaada mkubwa. Wanaokumbuka mara ya mwisho marehemu Tambwe Leya alipokuwa Jangwani alisajili vijana kina Kally Ongara na wengine ambao waliweza kufanya vizuri licha ya kuandaliwa kwa muda mfupi. Tuandae wengine sasa, matunda tutayaona.

3. Suala la timu/klabu kijitegemea lishughulikiwe mapema. Wanachama/wapenzi washirikishwe kuitegemeza klab/timu kupitia ada/hisa, etc.

Kwa muda huu wa mwaka mzima na zaidi ambapo mfadhili analipa mishahara ya makocha na wachezaji, tulitakiwa kuwa tumekusanya nguvu za kutosha ili hata kesho akisema fungu lake limeisha, tusilazimike kuwapigia magoti kila Sunday kayuni!

Zack,

Anonymous said...

Duh! Huyo mwenye picha inayoonyesha vidole vinne ana vidole vizuri sana. Hongera sana. Mkono soft kinoma.