Wednesday, April 09, 2008

Yanga na Manyema leo

Baada ya kutolewa katika michuano ya Kimataifa mwishoni mwa wiki, Yanga leo inarudi katika mawindo yake ya kuwania ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom wakati itakapopambana na Manyema FC kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar.

Yanga inahitaji ushindi wa mechi tatu tu kuanzia leo ili ifikishe pointi 52 na kujitangaza bingwa mpya wa Bara kwani hakuna timu inayoweza kufikia pointi hizo kwani Simba itaishia kwenye 51 hata ikiifunga Yanga Aprili 27.

Mechi hiyo ya Yanga haitazamiwi kuwa na ushindani mkubwa kutokana na udhaifu wa mpinzani wake, Manyema ingawa watabiri wa mambo wanasema inaweza ikawa kama ile ya Simba na Manyema timu hizo zilipotoka sare ya bila kufungana.

Kila la heri vijana wetu leo.

8 comments:

CM said...

mpira ni mapumziko na tunaongoza 1-0.

CM said...

dakika ya 47, Hamisi Yusuf anaipatia Yanga bao la pili.

Anonymous said...

ahsante tunaomba yanga ishinde mechi zote matokeo ya al akhdar yasipoteze baadhi ya mechi m sakran kuwait

CM said...

dk 55, Manyema wamepata bao la kwanza. Mvua imeanza kunyesha uwanjani.

Ni 2-1 sasa.

CM said...

dk 58 Abdi Kassim anaachia mkwaju na kuipitia Yanga bao la 3.

ni 3-1

Anonymous said...

waongeze presha tunataka zaidi ili vijana wasahau mechi iliopita m sakran

CM said...

Mpira umevunjika kufuatia mvua iliyonyesha

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___