Saturday, April 05, 2008

Dawa ya Waarabu bado
Kwa mara nyingine tena, Yanga imeshindwa kuitoa timu inayotoka katika nchi zenye asili ya Kiarabu baada ya kupokea kichapo cha 1-0 nyumbani licha ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuilazimisha Al Akhdar 1-1 huko Tripoli wiki mbili zilizopita.
Yanga ilipata nafasi ya kusawazisha bao hilo katika dakika ya 82 wakati ilipopata penati lakini mpigaji wake Hamisi Yusuf alipiga mpira ambao uliokolewa na kipa wa Al Akhdar.
Kwa mtaji huu basi, Yanga inarejea kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo inaelekea ukingoni.

3 comments:

Anonymous said...

Dawa ya waarabu ni kuandaa timu kisayansi. Sio kamati za ufundi za mzee Matunda na Mzimba!

1. Ile timu 'anayofundisha' Chamangwana (kama ipo) iko wapi maana sijaisikia ikicheza hata mechi moja. Hii ndio ingetoa wachezaji wa kusajiliwa Yanga msimu ujao, badala ya kuokoteza wachezaji waliochoka.

2. Na ile timu ya watoto ambayo ilikuwa ifundishwe na kocha toka Serbia ikowapi? Hii ingetoa wachezaji wa Yanga watakaoshindana na wenzao wa arabuni ktk miaka mi5 ijayo.

Badala yake viongozi watasema wako busy kuandaa timu kwa michezo ya kimataifa. (Sisemi haya sababu tumefungwa, bali kwa sababu naamini ndio njia pekee ya kupata mafanikio endelevu - sustainable growth and success, bila hivyo tutakuwa tunabahatisha tuu ushindi/sare moja, kisha tunafungwa mechi ambayo tulitakiwa kushinda).

Sielewi hadi leo kwa nini viongozi walikataa mapendekezo ya kuifanya timu iendeshwe kibiashara amabayo walikuwa wameyakubali wakati wanagombea. maana inabidi kuwe na watu walioajiriwa kuendesha timu, tofauti na sasa ambapo kuongoza timu za Yanga ni part time job.

Na lilezoezi la kuingiza wanachama wapya liliishia wapi?

Kama nilivyosema hapo awali, viongozi wanaoongoza klabu na timu on part time basis, wako overwhelmed na majukumu, kiasi kwamba hakuna kinachofanyika kikamilifu. Napendekeza tena, viongozi wa kuchaguliwa waongoze klab na shughuli zake, na timu iwe chini ya Manager wa kuajiriwa (kama Kondok) na huyu ariport kwa board yenye wajumbe wa kuajiriwa. Hawa wapewe malengo, na wasipoyatimiza, basi mlango watakuwa wanauona wenyewe.


Zack,

Anonymous said...

Tunaomba matokeo ya mecho ya ligi leo ... maana kuvunjika kwa koleo sii ...

Soccerssg said...

Analysis ya mchezo huu ingia hapa www.tuntucoach.blogspot.com