Saturday, April 05, 2008

Kufuzu au kutofuzu ni leo

TIMU ya Yanga leo inashuka dimbani ikiikaribisha Al-Akhdar ya Libya kumalizia ngwe ya mchezo wao wa marudiano katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF) utakafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa awali Yanga wiki mbili zilizopita, nchini Libya timu hizo zilifungana bao 1-1, hivyo Yanga leo inahitaji ushindi wa bao 1-0 au hata ikitoka 0-0 itasonga mbele.

Ingawa mashabiki wanaipa nafasi kubwa Yanga leo, lakini isibweteke kwani katika soka lolote linaweza kutokea hivyo kuharibu ndoto ya mashabiki wa Tanzania kuona timu yao ikisonga mbele.

Ni wazi kuwa Al-Akhdar nayo imejiandaa, itacheza kwa nguvu kuhakikisha inaibuka na ushindi.

Majaliwa ya mchezo wa leo yatategemea hali ya hewa, ambapo kutokana na mvua ambayo imenyesha leo asubuhi zinauweka katika wakati mgumu mchezo huo kutokana na uwanja huo kujaa maji. Hata hivyo kufikia saa nne leo asubuhi mvua ilikuwa imekata na hivyo kutoa matumaini ya kupigwa kwa mtanange huo.

Kila la heri wana Jangwani. Na kama kawaida mambo yakienda vizuri tutawasiliana hapo chini kwenye comments ili kupata yale yanayojiri ndani ya dakika 90.

19 comments:

Anonymous said...

nawatakia kila la kheri ktk mchezo wa leo ingawa nasikia uwanja umejaa maji inshaallah maji yasiharibu matokeo na tujulishane matokeo mdau wa yanga m sakran kuwait

Anonymous said...

mpira upo !!!!!
m sakran

Anonymous said...

dakika 34 zimeondoka hadi sasa bado 0-0.

Vijana wetu bado hawajafanikiwa kupeleka presha kubwa golini kwa wapinzani.

Anonymous said...

ahsante nawatakia kila la kheri vipi maji uwanjani

Anonymous said...

HT 0-0

Anonymous said...

Vipi maendeleo, kipindi cha kwanza si kitakuwa kimemalizika sasa?

Anonymous said...

OK, asante Vipi uchezaji..?

Anonymous said...

dk 57 tupo nyuma kwa 1-0

Anonymous said...

Al Akhdar wamepata bao baada ya kona iliyopigwa kutoka mashariki mwa uwanja kuunganishwa kwa kichwa na mcezaji mmoja wa Al Akhdar.

Tupo nyuma kwa bao 1.

CM

Anonymous said...

Hii ngoma tumelala sidhani kama tutatoka soka la Bongo UGOJWA WA MOYO

Anonymous said...

ohoo... keep us informed, tunatakiwa kurudisha hilo bao..

Anonymous said...

dakika ngapi sasa

Anonymous said...

naomba waongeze presha tunatak ala pili asante sana

CM said...

hamis Yusuf amekosa penati katika dk ya 82.

Inasikitisha kwa kweli.

CM

CM said...

KUMRADHI WADAU NILIKUWA NIMEANDAA SENTENSI KWAMBA HAMIS YUSUF AMEFUNGA PENALTI LAKINI GHAFLA KATIKA KU-CANCEL, VIDOLE VIKATELEZA NIKAJIKUTA NIMETUMA.

BADO TUPO NYUMA KWA 1-0. HIVI SASA NI DK.YA 88

Anonymous said...

nadhani tushaondoka

CM said...

TUMETOLEWA.

Mpira umekwisha kwa kipigo cha bao 1-0 nyumbani.

Kwa kweli mchezo ulikuwa mbovu sana kwa timu yetu.

Anonymous said...

ahsante kwa mawsiliano niliuona mpira wa kwanza libya nilikuwa na imani tutasonga mbele lakini mpira ni mduara unadunda tuelekeze nguvu ktk ligi poleni wana jangwani wote wenu mdau m sakran kuwait

Anonymous said...

Monday, 21 January 2008
BASILIUS NAMKAMBE
MWANAYANGA KUTOKA TAWI LA MAKUTI -MAGOMENI JIJINI DSM

Ya Kale Dhahabu! (1981-93)
Orodha ya wachezaji wa zamani wa timu ya soka ya Yanga, (watoto wa Jangwani) walioleta ushindi, makombe, sifa, burudani na pia kuleta mafanikio ya muda mrefu ktk timu (tangu nimeanza kuifahamu na kuishabikia Yanga 1980)!

tunataka viongozi na kocha katika msimu ujao watusajilie wachezaji wa dizaini kama hii waliopita na siyo wasiokuwa na uchungu na timu kama wengi wao wa sasa.

wakumbke wachezaji kama hawa-

Walinda mlango (Goal-Keepers)
1. Juma Pondamali
2. Joseph Fungo
3. Hamis Kinye
5. Steven Nemes

Mabeki wa kulia, na.2:
1. Juma Shaaban (Anko J)
2. Bakari Malima (Jembe Ulaya)
3. Ngandu Ramadhani
4.Yusuf Ismail Athumani ‘Bana’


Mabeki wa kushoto, no.3:
1. Ahmed Amasha (mathematician)
2. Kenneth Mkapa
3. Fred Felix Minziro (Majeshi)

Mabeki wa kati kulia, na.4:
1. Athumani Juma Chama
2. Alan Shomari
3. Willy Mtendamema

Beki 5 (mkoba)
1. Constantine Kimanda
2. Salum Kabunda (ninja)

Viungo wa kati, na.6 & na.8:
1. Juma Mkambi (Jenerali)
2. Isaack Mwakatika
3. Charles Boniface Mkwasa
4. Yusufu Macho
5. Salvatory Edward
6. Sekilojo Chambua
7. Shaaban Ramadhan

Viungo/washambuliaji wa kulia, na.7:
1. Charles Kilinda
2. Charles Alberto

Viungo/washambuliaji wa kushoto, na.11:
1. Sanifu Lazaro
2. Thomas Kipese
3. Edibily Jonas Lunyamila
4.Celestine ‘Sikinde’ Mbunga

Washambuliaji:
1.Rashid Hanzuruni
2. Omari Hussein (Kevin Keegan)
3. Makumbi Juma (Homa ya Jiji)
4. Abeid Mziba
5. Edgar Fongo
6. Said Mrisho (Zico wa Kilosa)
7. Said Mwamba (Kizota) jezi no.14
8. Said Suedi (Scud)
9. Mohamed Husein (Mmachinga)
10. Zamoyoni Mogella (dhl) 1992/93??
11. Hamis Gaga (Gaggarinho/Chiluba) 1992?
12.Kally Ongala

Yanga ya sasa ikumbuke historia ya klabu na kuienzi. Vijana waliopo waturudishie hiyo heshima ya enzi hizo.
Yapo mazuri yaliyotokea ktk klabu ya Yanga kabla ya 1980, na inafaa nayo yakubalike na kuenziwa - na kwa kweli sikuyabagua bali imenibidi nianzie pale ambapo mimi mwenyewe nilikuwa nafuatilia maendeleo ya Yanga.