Wednesday, April 23, 2008

Siku ya kuwakata maini Simba leo
Mabingwa Yanga leo inajitupa katika Uwaja wa Kaitaba huko Bukoba kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakati itakapopepetana na Kagera Sugar ya huko.

Ushindi kwa Yanga katika mchezo huo, utawakata kabisa maini klabu ya Simba ambayo inadai imekata rufaa katika Baraza la kusuluhisha masuala ya Michezo CAS kudai pointi zake 3 ilizonyang'anywa dhidi ya Coastal Union kwa kumchezesha Juma Said 'Nyoso' aliyekuwa ana adhabu ya kufungiwa. Yanga ikishinda mchezo huo itakuwa imejikusanyia pointi 51 wakati endapo Simba itashinda rufaa yake pamoja na kushinda michezo yake miwili iliyobaki itafikisha pointi 49.

Tungoje tuone jinsi Yanga itakavyopeleka kilio Msimbazi leo . Ikumbukwe kwamba ada ya kukata rufaa CAS ni dola za Kimarekani 10,000. Kazi ipo.


17 comments:

Anonymous said...

Kila la heri Yanga. Hata kama haiwezi kushinda kule Kaitaba, BK, Simba haina uhakika wa kushinda mechi zake zote. Ikumbukwe hatujacheza nao kwa hiyo ubingwa wetu uko salama kwa mazingira yoyote yale.
Hata rufaa yao hawana uhakika 100% kushinda!

Anonymous said...

matokeo vipi ? bado hamjapata habari m sakran kuwait

CM said...

tupo nyuma kwa 2-0 dakika ni ya 57 sasa.

CM said...

mambo si mambo. Tumepigwa bao la tatu.

Hata hivyo hapa Dar es Salaam ni dakika za majeruhi na Simba imeng'ang'aniwa na Polisi Dodoma 2-2.

Anonymous said...

kidogo tutapumua iwapo simba nao watapoteza mechi yaleo

Anonymous said...

tujulisheni matokeo ya mechi zote za leo yaani ya dar na bukoba m sakran kuwait

CM said...

Mpira umekwisha hapa Dar kwa sare ya 2-2.

Simba sasa imefikisha pointi 41.

Anonymous said...

sasa wasahau hata nafasi ya pili inshaallah mechi tuwazibue tuone rufaa yao itawapeleka wapi m sakran

CM said...

Mpira umekwisha huko Bukoba kwa kipigo cha 3-1.

Hii ni mechi ya kwanza ya ligi kwa Dusan Kondic kuipoteza.

Tumebaki na pointi zetu 48 ambazo kwa uhakika sasa haziwezi kufikiwa na timu yeyote.

Kagera Sugar 3 Yanga 1

Anonymous said...

kufungwa ni sehemu ya mchezo muhimu kujipanga upya kumtungua mnyama ili midomo izibwe kila tufunguapo magazeti wao wana uwezo wa kumfunga yanga inshaallah mara hii iwe ndio mwisho wao m sakran

Anonymous said...

mmeona kikosi kilichocheza, sasa nafikiri tuheshimu upangaji wa kocha. Waliocheza leo wengi ni kikosi cha pili

Anonymous said...

Ndugu wadau kumradhi kwa kuwa kimya. Hivi sasa nipo U'Taifa kuwaletea yale yanayojiri. Kaeni chonjo

Anonymous said...

Tumekaa mkao wa kula, kwanza tupe line up za timu zote mbili

Anonymous said...

HT:0-0 wadau network inasumbua sana.

Anonymous said...

jamaa sie tunasubiri matokeo hukoo
m sakran kuwait

Anonymous said...

Hongera hongera wana yanga ngoma drew 0-0 redio bbc maelezo zaidi kwenu watu wa nyumbani m sakran kuwait

Anonymous said...

sasa kama Simba haikuwakilishwa na kikosi chake cha kwanza, na kusimamisha wachezaji wote bado wametuzuia kufunga? kweli timu inahitaji ukarabati mkubwa