Tuesday, June 17, 2008

Mahadhi na wengine 8 waachwa Jangwani
Waziri Mahadhi

Waziri Mahadhi "Mendieta" ni miongoni mwa wachezaji 9 walioachwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya usajili wa msimu ujao wa ligi.

Akitangaza majina hayo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Lucas Kisasa amewataja wachezaji wengine walioachwa kuwa ni Benjamin Haule, Jackson Chove, Lulanga Mapunda, Hussein Sued, Gula Joshua, Abuu Ramadhani, Aime Lukunku (kutoka DRC) na James Chilapondwa (kutoka Malawi).

Kutangazwa kwa majina hayo kunafuatia masharti yaliyotolewa na Shirikisho la soka nchini TFF kwamba klabu zinatakiwa kutangaza mapema wachezaji watakaowaacha ili zoezi usajili liweze kuendelea katika hatua ya pili ya uhamisho wa wachezaji.

Kuachwa kwa Mahadhi huenda kukatokana na mchezaji huyo kipenzi wa Jangwani kuwa majeruhi kwa muda mrefu. Hali kama hiyo huenda ndiyo imesababisha mchezaji James Chilapondwa kutoka Malawi kuachwa kwani msimu mzima hajaonekana dimbani.

Mchezaji ambaye amekuwa akizungumzwa na wengi kuwa ataachwa katika msimu ujao wa ligi Gaudence Mwaikimba bado yupo katika wachezaji watakaoendelea kukipiga katika klabu hiyo. Kiwango cha Mwaikimba kimeonekana kushuka sana tangu kuja kwa kocha Milutin "Micho" na hali hiyo kuendelea kwa kocha wa sasa Dusan Kondic.

Imeelezwa kwamba wachezaji wote waliobakia wamesaini isipokuwa Abdi Kassim ambaye bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo.


11 comments:

Anonymous said...

Kwa kiasi kikubwa, nakubaliana na uamuzi wa kuwaacha wengi kati ya hao tisa, lakini, with due respect to Kondic, naomba kutofautiana kuhusu kuachwa kwa Gulla Joshua. Gulla, kimsingi, ni mzuri sana; ana kasi, umiliki wa mpira, anajituma, etc. Kilichomponza ni kukaa benchi muda mrefu kutokana na maumivu. Nilidhani kwamba angetulia na kupewa nafasi, angerudi kwenye kiwango chake. Believe me, ukimwondoa Mwalala, hakuna mchezaji katika safu ya ushambuliaji ya Yanga, aliye mgumu kumkaba kama Gulla. Alipokuwa anatumika kama sub, alikuwa anabadili kabisa sura ya mchezo kutokana na kasi yake na nidhamu ya kufuata maelekezo. Na ndiyo kwanza amepona na alikuwa anaanza kurudi kwenye kiwango! Surely, hatujamtendea haki. Nadhani historria itakuja kutusuta, kama ilivyofanya kwa Banka ambaye baada ya kuumia na kushuka kiwango tukamwacha lakini sasa anavutia sana kumwangalia jinsi anavyotawala kiungo cha Simba mpaka viongozi wetu wakataka kumsajili tena mwaka huu! Mwingine ambaye kwa maoni yangu angebaki ni Jackson Chove. Ni mrefu na makini golini; nakumbuka jinsi alivyoziba pengo la Ivo na Benja katika raundi ya kwanza ya ligi mwaka huu.

Kwa upande mwingine, nilitegemea mwalimu angewaacha Credo, Mtiro (anacheza mpira wa kitoto-kanzu, danadana na vitu visivyokuwa na manufaa), Hamis (uwezo wake wa kumiliki mpira na kutoa pasi ni wa chini mno!) na Mwalala (ni msumbufu sana). Pia angeweza kumruhusu Amir Maftah atafute timu nyingine hasa baada ya kuwapata Stephano Mwasika na Nurdin Bakari. Najua wengi watatofautiana na mimi, lakini kwa waliofuatilia kwa makini uchezaji wa Maftah katika Yanga watagundua kuwa kijana huyu haendani na mfumo wa uchezaji wa Yanga kwani huwa anapwaya mno na hawezi kupeleka mashambulizi mbele. Hakabi, anapoteza sana mipira, anapitika kirahisi, hana concentration na ni mvivu. Natambua kuwa ana vitu fulani vinavyomtofautisha na wachezaji wengine wa nafasi yake-hasa ujana na kujifunza mpira tangu utotoni kwenye club ya Rollingsone ya Arusha(nadhani ndivyo vinayomvutia Maximo) lakini kwa Yanga ameshindwa ku-deliver. Hata Chelsea walitambua kuwa Damian Duff, Assier Del Horno na Glen Johnson hawakuwa wakiendana na mfumo wa kocha ingawa walikuwa wazuri sana (!), hivyo wakawauza. wakawauza.

Anonymous said...

bro very good comments ,nadhani sasa hivi yanga wanafanya vitu kuwakomoa simba.

Anonymous said...

I like the analysis ingawaje siko nyumbani sijaona uchezaji wao but it is well documented bravo brother

Anonymous said...

Mdau wa kwanza hapo juu ametoa analysis nzuri. Natofautiana kidogo juu ya kuachwa kwa Gulla na Waziri Mahadhi. Kama mchezaji ameumia muda mrefu, kumbakiza Yanga hakutamsaidia sana. Anahitaji atoke, apate timu itakayomtumia na kumrudisha kwenye form, then Yanga watamfuata tena. Mfano wa Banka ni mzuri.

Ni vigumu kwa mchezaji aliyekaa benchi muda mrefu kurudi kwenye form yake akiwa Yanga, maana kila msimu wanasajiliwa wapya, hivyo hakuna muda wa kumpa nafasi majeruhi.

Kitu kingine ni kuwa sio wote ambao hawajatajwa watakuwepo Jangwani msimu ujao. Mfano ni Vicent Barnabas ambaye nasikia amerudi Kagera Sugar. Wapo wengine watakaouzwa kabla msimu wa usajili haujaisha. Sitashangaa kusikia kina Mwaikimba, Mwalala, etc hawapo.

Anonymous said...

waziri mahadhi kapewa timu under 20 kuikochi according to todays yanga newspaper.

Anonymous said...

Nsajigwa amesaini Simba.Hii vita naona haitusaidii chochote.Tusajili wachezaji watakaotusaidia.Kaseja kulipwa mapesa na kukubaliwa mkataba unaosema yeye atakuwa kipa namba moja ni ujinga uliokithiri.Je aki drop form???Mkataba uvunjike???Tutajuta kwa mikataba ya kijinga tulioingia na wachezaji mamluki.

Masebe said...

Usajili huu ni wa kipuuzi kabisa.Nilitegemea kuwa watatafuta washambuliaji wazuri toka nje ya nchi kwa ajili ya Champions leqeu, lakini inashangaza kuhangaika na wachezaji wa hapa ambao hawapishani viwango, mwisho wa siku tunatolewa mapema kwenye mashindano kwa kukosa wafungaji.Huu ni ujinga mkubwa.

Anonymous said...

Nafikiri kuna matumizi mabaya ya fedha. Fedha hizi zingetumika vizuri tungeweza kuwa na timu nzuri sana, lakini kwa sababu tunatumia fedha kuwakomoa simba inasikitisha mno.Hawa mamluki tunaochukua wenyewe tena kwa fedha nyingi hivyo watatusaidia nini.Akina Ivo walifungiwa kwa madai ya kuihujumu timu,inakuwaje tunaongeza kundi la wahujumu tena kwa gharama kubwa hivyo? Haiingii akilini kabisa. Kama klabu ina fedha kiasi hicho kwanini wasitafute wachezaji wa kulipwa toka nje ya nchi hasa forwad badala ya kuhangaika na hawa ambao viwango ni vya chini? Fedha zipo ila mipango ni zero kabisa.

Anonymous said...

Ndugu zangu hizi zana za kuwa huyu Simba au Yanga damu zimepitwa na wakati. Hakuna mchezaji ambaye yeye ni damu na timu fulani ikifikia hivyo huyo amekosa profetionalism na timu za nje zikimjua hatauzika. Kama kocha anamtaka mchezaje ni yeye anayejua formation gani anataka timu icheze, tuache ushabiki wa kitoto kuwa hawa mamluki hizi zana zinatoka wapi? mpira si chama cha siasa.

Anonymous said...

Wajameni,
Hivi hii itikadi ya mamluki mnaitoa wapi? kwani leo hii wachezaji wameanza kuhama kutoka Simba kwenda Yanga au kutoka Yanga kwenda Simba? mnamkumbuka Zomoyoni Mogela? Yusuf Bana? hawa hawakuma Simba na kuichezea Yanga kwa uadilifu? huu ni mfano mchache tu, wachezaji kwa kawaida hawana timu wanakwenda pale anapohitajika, yeye kwake hii ni ajira.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___