Tuesday, June 10, 2008

Nurdin, Sued nao ndani!

Nurdin Bakari na Said Sued

Katika hali inayoonyesha hali ya mambo si shwari, klabu ya Simba imezidi kubomolewa baada ya habari kwamba wachezaji Nurdin Bakari na Said Sued nao wametua Jangwani.

Nurdin Bakari pamoja na Said Sued hawakumaliza msimu uliopita vizuri katika klabu yao ya zamani baada ya wao na wenzao wanne kufungiwa kwa utovu wa nidhamu.

Kusajiliwa kwa wachezaji hao kunafanya klabu hiyo kutimiza jumla ya wachezaji watatu kutoka Simba ambao wametua Jangwani. Juzi Yanga ilimsainisha nahodha wa klabu ya Simba Juma Kaseja kwa ajili ya msimu ujao.

Kundi la Friends of Simba ambalo linaratibu usjili wa Klabu ya Simba sasa linaonekana kuzidiwa nguvu licha ya kuanza vizuri kampeni yake ya usajili kwa kuwasainisha wachezaji Henry Joseph na Kelvin Yondani ambao nao walikuwa wakifukuziwa na Yanga.

Kazi ipo mwaka huu!

6 comments:

Anonymous said...

Nina mashaka kama tunasajili kwa lengo la kuimarisha timu. Inaonekana kama vile lengo ni kuikomoa Simba. Kitendo cha kuchukua wachezaji zaidi ya watatu kutoka timu moja is not healthy for our team. Ni vizuri tukaepuka kulundika mamluki ndani ya team. Nina hakika, tukija kufungwa na Simba wachezaji hawa watakuwa watuhumiwa wa kwanza.

Mpaka sasa wamesajiliwa Kaseja, Swed, Owino, Nurdin na Mwakingwe. Tunaambiwa pia wanakuja Banka na Machupa. Najiuliza watacheza namba zipi?! Midfield kuna Chuji, Mumbala, Kabanda, Abdi, Bonny, etc. Tuache upuuzi huu.

Anonymous said...

mzee,nakuunga mkono kabisa katika wazo lako.Lakini kumbuka katika mtazamo wa international matches(Champions League ya Africa)unahitaji kuwa na wachezaji ambao wako tayari muda wowote,hasa ukizingatia na ligi ya ndani itakua inaendelea,hivyo wachezaji usipokua na wachezaji wengi waliokua tayari,utapata majeruhi huku wakatio utakua unakabiliwa na mechi ngumu mbele yako.Hivyo nafikiri kocha amefikiria hicho,na pia kuwa na wachezaji wawili wa uhakika katika kila namba.Wazo langu la pili ni kuwa,Yanga wanatakiwa kutafuta suluhisho la tatizo la ushambuliaji,kwani ni ugonjwa wa Taifa,nashauri waende hata nchi za magharibi kama vipi,wakalete hata washambuliaji wawili tu wa uhakika.Tutakua tumepata dawa ya tatizo sugu kwani mid fielders tunao tena wa kutosha mwaka huu,hapo KONDIC nampa BIG UP.

Anonymous said...

tukae chonjo yanga sio zile hela zilizotumika kuwasajili hawa wachezaji ikaleta ugonjwa wa blood pressure kwenye klabu yetu.

Anonymous said...

Nafurahi kuwa wapenzi hapa bloguni wana-worry na hizi habari usajili. Jamani tusifurahie tuu kuikomoa Simba, tuangalie pia na sustainability ya hawa wachezaji. Nasikia wote wanasign mkataba wa mwaka mmoja. Kwa Tanzania kulipwa $30,000 kwa mkataba wa mwaka mmoja sio kitu cha kawaida.

Hapo msisahau kuna kufungiwa miezi 6 na kasheshe zingine za uhamisho kat ya Simba na Yanga; kwa hiyo hadi mchezaji anakuja kutulia uwanjani, imebaki miezi 6 mwaka uishe!

Ningefurahi zaidi kama usajili ungelenga wachezaji tutakaokuwa nao kwa miaka 3-4 ijayo, kina Makassy, nk.

Anonymous said...

Ni kweli unachokisema,tuangalie sustainability ya hawa wachezaji,lakini pia lazima ukumbuke kuwa hawa wachezaji wanamalengo yao ya mpira sio kukomea Yanga na pia wanaangalia maslahi.Ukisaini mkataba wa muda mrefu una madhara yake pindi maslahi ya wachezaji yanapopanda hauwezi kudai uongezwe.Kumbuka soka ni ajira na biashara pia

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___