Monday, June 09, 2008

Ni kweli!
Hatimaye imethibika kwamba Kipa wa Simba, Juma Kaseja amesaini kuichezea timu ya Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar, Kaseja alisikika akikiri kusaini mkataba huo licha ya kutomaliza mkataba wake na klabu yake ya zamani. Kaseja aliongeza kwamba hajagombana na mtu katika klabu ya Simba na anahama klabu hiyo kama walivyo wafanyakazi wanaohama kampuni moja kwenda nyingine, hivyo anaomba mashabiki wa Simba wamuelewe. Hata hivyo Kaseja amesema amewaachia viongozi wa klabu hizo mbili pamoja na TFF kumalizia suala hilo.

Alipoulizwa juu ya kupigania namba Jangwani, Kaseja amesema mkataba wake umeweka wazi kwamba yeye ndiye atakuwa kipa namba moja wa timu hiyo. Kuhusu suala la ugomvi wake na Athuman Iddy "Chuji", Kaseja amesema kwamba suala hilo huwa linakuzwa tu kwani huwa anakutana mara kwa mara na Chuji na hawana ugomvi kama inavyoelezwa.

Suala la kusajiliwa kwa Kaseja kunaendeleza migogoro ya mara kwa mara ya vilabu vya Simba na Yanga kupigania wachezaji.

Wakati huo huo, Yanga pia imemsainisha kiungo chipukizi wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars Kiggi Makassy kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.


4 comments:

Anonymous said...

kumbe siku zote viongozi wa Simba walikuwa hawajapeleka mkataba wa Kaseja TFF kwa ajili ya kusajiliwa?

Lakini hela iliyotumika kumsajili huyu kipa si ya kitoto. Tunaambiwa jamaa kakunja dola 30,000. SI mchezo.

Anonymous said...

Sijawahi kusikia mkataba wa mchezaji unasema huyu ndio atakuwa na namba ya kwanza ktk timu. Uhakika wa namba unatakiwa kuwa jitihada za mchezaji mwenyewe. Kocha ndio anatakiwa kuamua nani awe kipa wa kwanza sii mkataba! Ina maana kiwango kikishuka akawekwa benchi, atavunja mkataba? Au apangwe tuu kwa vile mkataba umesema hivyo.

This whole Kaseja transfer sounds like a hoax! Ila tunamkaribisha kama amekuja Jangwani kwa mikono miwili.

Anonymous said...

Acha imani za kizamani mzee,masharti katika mkataba ni kitu cha kawaidana mchezaji anatoa masharti kulingana na maslahi yake.Usitegemee,aseme kila kitu kukufurahisha,soka haiendi hivyo,na hiyo pesa unayoishangaa ni kidogo sana.Golikipa wa Petro Atletico ya Angola iliyokuja kucheza na Yanga, mshahara wake wa mwezi ulikua sawa na mishahara ya wachezaji wote waliosajiliwa na Yanga kwa mwezi.Hii ndio soka ya kulipwa mnayoililia kila siku,hivyo msianze kulalama na kushangaa kiasi hicho kidogo.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___