Tuesday, June 03, 2008

TAIFA STARS SPECIAL

Tutoke vipi?
L-R Waliosimama: Mrwanda, Nadir, Sued, Gabriel, H. Joseph. Walioinama L-R
Mbuna, Bonny, Ulimboka, Nizar, Maftah. Mbele ni Ivo Mapunda
(Picture from Michuzijnr blog)

Watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi timu yao imeshindwa kutoka uwanjani na ushindi katika mechi yake ya ufunguzi wa kampeni ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na ile ya Kombe la Dunia dhidi ya Mauritius Jumamosi iliyopita.

Je wewe kama mdau wa soka la Tz unasemaje? Tufanye nini ili tuwe washindani kweli?


2 comments:

Anonymous said...

pamoja na kwamba Amir Maftah ni mchezaji wetu, lakini kiwango chake inabidi tukitupie macho kidogo.

Katika siku za hivi karibuni Maftah hajaweza kucheza kwa kiwango cha kuridhisha na mara nyingi anajisahau sana uwanjani.

Pia ni bora aanze Chuji kuliko Nizar.

Anonymous said...

tusubiri tuone