Friday, June 06, 2008

TAIFA STARS SPECIAL
Sala zetu hukoo Cape Verde

Taifa Stars itajitupa uwanjani huko Praia, Cape Verde kupambana na timu ya Taifa ya nchi hiyo katika mchezo wa Kundi la 1 la kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na Kombe la Dunia 2010.

Pambano hilo litakalopigwa Jumamosi jioni (saa 12 za TZ), linatarajiwa kuwa gumu hasa ikizingatiwa kwamba Cape Verde itataka kurejesha imani yake kwa mashabiki wake baada ya kuonja kichapo cha 2-0 wiki mbili zilizopita kutoka kwa Cameroon.

Taifa Stars nayo imeondoka huku Watanzania wakiwa na wasiwasi katika safu yake ya ushambuliaji ambayo ilikosa mabao mengi ya wazi wiki iliyopita dhidi ya Mauritius.

Lakini pamoja ya yote hayo, sala zote ni kwa Taifa Stars. Mungu Ibariki TZ.

14 comments:

CM said...

mechi itaanza saa 2 usiku kwa saa za TZ

Anonymous said...

KIKOSI KITAKACHOANZA LEO:Ivo,Nsajigwa,Maftah,Sued, Nadir,Bonny,Iddi,Nizar,Henry, Gabriel,Mrwanda.

Anonymous said...

Tutasubiri matokeo hapa.

CM said...

Halftime: 0-0

Anonymous said...

Kikosi chetu kiko hivi

* (GK) Ivo MAPUNDA 1
* Meshack ABEL 2
* Amir MAFTAH 3
* Nadir HAROUB 4
* Salum SWED 5
* George OSSEY 6
* Athuman IDDY 10
* Yellow Card Emanuel GABRIEL 11 dk ya 32
* Nizar KHALFAN 12
* Geofrey BONY 17
* Uhuru SELEMAN 18

Anonymous said...

Kipindi cha pili kimeanza bado ni 0-0

Anonymous said...

anon wa 9:02PM hapo juu naona hiyo list ina walakini kidogo. List iliyotolewa mapema ndiyo iliyopo uwanjani.

Anonymous said...

Wewe Anon hapo juu data kamili hizo toka FIFA.com, mpira ni dk ya 65 bado 0-0, list ndio hiyo ya hapo juu sijui kaitowa wapi?

Habari zaidi cheki hapa

http://www.fifa.com/worldcup/preliminaries/africa/matches/round=250418/match=300036584/index.html

CM said...

tumefungwa bao katika dakika ya 72.

Anonymous said...

Mpira ni dk. ya 67 tumechapwa bao la kwanza, tuko nyma 1-0

Anonymous said...

Taifa Stars hakuna mchezaji anayeitwa George Ossey. Meshack Abel hajasafiri na timu (amebaki TZ).Uhuru Suleiman yupo benchi.

Anonymous said...

Mpira umekwisha tumelala 1-0 kwa kweli sidhani kama tutashinda mechi hata moja maana timu haina washambuliaji kabisa.

CM said...

Mpira umekwisha hivi punde na tumechapwa 1-0.

Mpira ulikuwa unatangazwa moja kwa moja na TBC.

Kwa matokeo hayo TZ imebakiwa na pointi 1 na tunakabiliwa na mechi ngumu wiki ijayo dhidi ya Cameroon.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___