Wednesday, July 23, 2008

KAGAME CUP
Mtihani wa V
ital'O leo

Mabingwa wa soka Tanzania Yanga leo wanaingia uwanjani kupepetana na Vital'O ya Burundi katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Kagame litakalopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kazi kubwa ya kuwaridhisha mashabiki wake ambao kuanzia jana jioni wameshindwa "kunywa maji" kutokana na tambo wanazipata kutoka kwa watani wao Simba ambao waliishindilia APR ya Rwanda kwa 2-0 katika mchezo mwingine wa robo fainali uliopigwa hapo jana.

Kutolewa kwa Yanga leo hii itakuwa ni pigo kubwa hasa ukizingatia kiasi cha fedha kilichotumika katika kusajili kikosi hicho kitakachoteremka dimbani kuumana na Vital'O ambayo ilishika nafasi ya tatu katika kundi A.

Mchezaji pekee ambaye yupo katika hatihati ya kucheza ni Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye licha ya kucheza mchezo uliopita dhidi ya Miembeni, bado anaonekana hajapona vizuri kwa ajili ya pambano la leo.

Tusubiri tuone mambo yatakavyokuwa leo. Kila la heri wana Jangwani.

Mechi za leo:

(1345hrs) Tusker vs Rayon
(1600hrs) Yanga vs Vital'O


27 comments:

Anonymous said...

kama sikusei huko nyumbani sasa ni saa kumi kasoro 5 wadau tupe mambo yalivyo huko wanjani.

Anonymous said...

mambo mpwito mpwito

CM said...

Dakika ni ya 13 tunaongoza kwa 1-0 bao limefungwa na Kiggi Makassy.

KIKOSI CHA YANGA:
1. Juma Kaseja
2. Fred Mbuna
3. Nurdin Bakari
4. Wisdom Ndhlovu
5. George Owino
6. Geo Bonny
7. Mrisho Ngassa
8. Shamte Ally
9. Boniface Ambani
10. Abdi Kassim
11. Kiggi Makassy

Anonymous said...

HII RAHA TUPU.

Anonymous said...

dk ya ngapi sasa? hilo moja bado limesimama? mashambulizi yakoje?

CM said...

Dakika ya 20, tumepata bao la pili kupitia kwa Boniface Ambani.

Ni 2-0 sasa mapemaaaa!

Anonymous said...

walete walete!!! hii blog utadhani niko daslama. mechi nafuatilia LIVE mweeee!!!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

ASANTEEEEEE

Anonymous said...

VIPI MATCH YA KWANZA?

Anonymous said...

weweeeeeeeeeee

Anonymous said...

nilikuwa sijui kwamba vital'o nao ni simba... nimeona nembo yao hapo juu nikagundua.. ish kumbe nao ni wanyama! wacha tuwakobange sasa. naomba tuwakomelee mengine ma2

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

imekuwaje?tena hawa jamaa kusawazisha?

Anonymous said...

au 2-2 ni matokeo ya mechi ya kwanza?

CM said...

Dakika ni ya 70 bado tunaongoza 2-0.

Anonymous said...

wacha utani hakuna 2-2 bado ni 2-0

Anonymous said...

EVERY COMMENT SHOULD BE FILTERED BEFORE GETTING POSTED, TO KEEP OTHER PEOPLE WHO ARE NOT ETHICAL,TO WRITE STUPID THINGS.

Anonymous said...

Says who punk????

Anonymous said...

mpaka dakika hii tumeshuhudia watu wastaarabu wakiweka comment zao hapa bila filter wala nini. sasa mtu anapoanza kuleta pollution zake hapa itabidi kweli chekecheo liwekwe

CM said...

Tupo kwenye stoppage time. 3 miuntes added

matako makubwa said...
This comment has been removed by the author.
CM said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-0.

Yanga sasa itakumbana na Tusker Ijumaa katika nusu fainali.

Tusker iliitoa Rayon kwa penati 7-6 mapema leo.

Alamsiki

Anonymous said...

Jamani sasa tena mtu unaitwa matako makubwa kwi kwi huko uarabuni unasalimika kweli???

Anonymous said...

Mdau wa Kuwait na hilo jina lako kaa huko huko utatajirika.

Anonymous said...

Sitashangaa ukikutana na huyu mdau wa kuwai, nina uhakika akihema tu anapumlia kote kote ha ha ha. Lakini Unguja anaweza kukaa hako kamchezo kanapendwa pale anzia Karume mkubwa, maalim Seif

Anonymous said...

Yangu, kwa ajili ya wanayangu na wapenda michezo wote popote duniani. Hii inatia laha ndani ya loho kama tunapata mafanikio kama hivi. Ila nawaomba wadau wote tulioko nchi ya nje hivi tujijitolea kila mtu dola 10 kama tuko milioni 2 wanayanga tutapata dola 20,000 kwa ajili ya kuchangia uwanja wetu uweze kutengezezwa vizuri katika hazi inayo takiwa.

Anonymous said...

hebu piga hesabu vizuri kaka.