Sunday, July 06, 2008

Kikosi hadharani keshoGeorge Owino

Kikosi kipya cha Yanga kinatarajiwa kujitupa kwenye uwanja wa Taifa kesho (7/7) kupambana na Express ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu.


Yanga inatarajiwa kuweka hadharani kwa mara ya kwanza wachezaji wake wapya akiwemo yule anayesubiriwa sana - Juma Kaseja ambaye amesajiliwa kwa mamilioni ya fedha kutoka kwa Simba.


Wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kuonekana katika jezi ya Yanga ni Nurdin Bakari, Geoffrey Bonny, George Owino, Kiggi Makasy na yosso watatu ambao wamepandishwa kutoka katika kikosi cha pili (Black Stars) kilichokuwa kinanolewa na Jack Chamangwana.


Express wapo nchini kwa mwaliko wa Chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA) na hapo jana walicheza na Simba na kutunguliwa 1-0.

5 comments:

Anonymous said...

wadau mpira umeishaje

Anonymous said...

Express 4 Yanga mgongo wazi 0

Anonymous said...

Ya kweli hayo?

Anonymous said...

we oota tu.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___