BAADA ya jana kuishuhudia Simba ikilizwa mabao 3-2 na Tusker ya Kenya, leo ni zamu ya Yanga kuwakabili mabingwa watetezi, APR ya Rwanda katika mchezo wa Kundi C utakaofanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa.
Yanga, ikiwa na silaha zake zilizoandaliwa mahsusi kwa michuano hiyo na ile ya kimataifa itaingia kwenye uwanja kwa tahadhari kubwa. Golini anatarajiwa kuwa Juma Kaseja ambaye atalindwa na ngome itakayoongozwa na Wisdom Ndhlovu na George Owino. Bila shaka katika ushambuliaji kutakuwa na kazi kubwa katika upangaji kwani Yanga kwa sasa ina washambuliaji wengi walio katika hali nzuri ya kimchezo.
Yanga, ambayo katika michezo ya kujinoa iliilaza Express ya Uganda kwa bao 1-0 na pia kuizima Mbagala Market kwa mabao 2-0, inabeba jukumu la kuanza vizuri ili kurejea imani ya mashabiki wake na Watanzania.
Lakini, Yanga inatarajia upinzani mkali kutoka kwa vijana wa APR, ambayo kwa sasa inanolewa na Mholanzi Renne Feller na inajivunia mshambuliaji wao hatari Haruna Niyonzima.
APR, ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii waliwasili nchini wakidai kuwa wametumwa na Rais Kagame warejee Kigali na kombe hilo.
Tusubiri tuone hizo dk 90 .
7 comments:
Mkuu tupe matokeo na tathmini ya mechi ya APR
bado mapema hata mechi haijaanza, labda atupe line up ikoje?
vipi huko
Naji ya shingo.
MAJI
Jamani tuambieni kinachoendelea, hayo maneno ya maji ya shingo hayasaidii
APR 2 Yanga 2
Post a Comment