Friday, August 22, 2008

Ligi kuu 2008/09 kuanza leo

Msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara 2008/09 unatarajiwa kuanza leo kwa mapambano mawili ya ufunguzi.

Simba leo itaumana na Villa Squad ambayo ni timu ngeni katika ligi hiyo, mpambano utakaopigwa katika uwanja wa zamani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Pia Kagera Sugar itaikaribisha Polisi Mororgoro kwenye UWanja wa Kaitaba huko Bukoba.

Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na kituo cha televisheni cha kulipia cha GTV, inatarajiwa kushirikisha timu 12.

Timu hizo ni Yanga, Simba, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Toto Africa na Polisi Morogoro.

Timu nyingine katika ligi hiyo ni Polisi Dodoma, Villa Squad, Azam FC, Moro United, Kagera Sugar na JKT Ruvu.

Yanga itaanza kampeni yake ya kutetea ubingwa huo kwa kupambana na Tanzania Prisons keshokutwa katika Uwanja wa Taifa wa zamani.

3 comments:

Anonymous said...

Matokeo vipi? Tupe hata hayo ya ki-mnyama...

Anonymous said...

Simba wameshinda 4-1. Kagera Sugar nayo imeshinda 2-0

Anonymous said...

Bomba, safi sana. Tunasubiri jpili ..