Sunday, August 24, 2008

Utetezi kuanza leo
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara - Yanga leo wanaanza kampeni yao ya kutetea ubingwa huo kwa kuikaribisha Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Katika msimu uliopita timu hizo mbili ndizo zilizomaliza msimu kwa kushika nafasi mbili za juu hali inayoonyesha ubora wa mchezo huo hii leo. Hata hivyo Prisons imepoteza wachezaji wake wawili mahiri waliotamba msimu uliopita - Geofrey Bonny (aliyejiunga na Yanga) na Stephano Mwasika (aliyetimkia Uarabuni), aidha kocha wa timu hiyo John Mwambusi naye ameshindwa kuelewana na timu hiyo kuhusu mkataba wa kuendelea kuinoa timu hiyo. Yanga inaonekana imejiimarisha kwa kufanya usajili wa mamilioni ya fedha msimu huu.

Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana Jijini Dar es Salaam, matokeo yalikuwa sare ya 2-2. Huku mabao yote ya Prisons yakifungwa na Geofrey Bonny.

Matokeo ya mechi za jana za ligi hiyo:
Moro United vs Azam FC.....................3-2
Toto Africa vs JKT Ruvu .....................1-0
Mtibwa Sugar vs Polisi Dodoma............0-0

7 comments:

Anonymous said...

Ni halftime sasa tunaongoza 2-0.

Mwalala & Ambani

Anonymous said...

kimya?

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 4-0

Anonymous said...

Tupeni majina ya wafungaji wa magoli yote wajameni

CM said...

Magoli ya Yanga katika mchezo wa leo yalifungwa na Ambani (mabao 2), Mwalala na Athumani Iddi Chuji.

Anonymous said...

YANGA mwendo mdundo mwanzo kama wa CHELSEA ....... mbona watako mwaka huu....

Anonymous said...

wajameni tuangalie sana hawa jamaa wa Simba ivo hamuoni wamejitengenezea kamtandao kwa sasa?

naona vimatawi vyao kama wamevirudisha!!!

ebu angalia Vila squad nature yake, then nenda Azam kisha urudi Moro United.

halafu wamejipanga mnno kwenye chaguzi za TFF Mikoani ambako wameshinda maerneo mengi ili waje mwezi wa 12 kushinda pale TFF.

SASA KWA UPANDE WETU UJUE HUWA NJAA ZA MAKOMANDOO WETU ZINATUZINGUA YAANI UTAWAKUTA WAKATI WA KAMPENI UCHAGUZI WA TFF WANAWASHABIKIA AKINA MAGORI WAPITE!!!!

MFANO BWANA MDEKA ALIKUWA MPAMBE WA MAGORI AMBAYE LEO ANATUCHEFUA.